Kenya: Pacha wawili waomba kuolewa na mwanaume mmoja ili wasitenganishwe. Jamaa akubali kuwaoa

Kenya: Pacha wawili waomba kuolewa na mwanaume mmoja ili wasitenganishwe. Jamaa akubali kuwaoa

Kwahiyo hao ndo wana wa 3some eeh!! Wanafaidi sana,

Huna ubabu wowote acheni kutunyima ambavyo hatujawaomba🙊🙊

Hauwezi kumnyima mtu kitu usichokua nacho, harakati zilishafika tamati. Muda wetu imeisha, Kwa Sasa tunajitahidi Milo yenye mboga mboga, matunda Kwa wingi na mazoezi ya hapa na pale.

Hao jamaa ndio wataalam wenyewe waasisi kabisa tena wana hati miliki.
 
Hauwezi kumnyima mtu kitu usichokua nacho, harakati zilishafika tamati. Muda wetu imeisha, Kwa Sasa tunajitahidi Milo yenye mboga mboga, matunda Kwa wingi na mazoezi ya hapa na pale.

Hao jamaa ndio wataalam wenyewe waasisi kabisa tena wana hati miliki.
Simu yangu haina chaji na umeme umekatika babu, nitarudi baadae
 
Nilishuhudia mshkaji mmoja alitaka kuoa na mchumba akasema siwezi kumuacha rafiki wa damu damu, tulieishi tangu utoto kwa hiyo tuoe wote
Jamaa akawaoa wote 2
Tatizo likaanza walipochangia mme
Haikufika hata miaka miwili, mmoja wao akasema nimechoka ku share mme
Akaomba talaka mwenyewe
Nafikiria tu na sio mchawi
Niko hapa

Mii wasiwasi wangu, wanapokuwa na umoja inakuwa sawa una mke mmoja. Maana hakuna ushindani ambao huongeza ubora. Kwa zamani ingekuwa bomba sana, ila kwa sasa inapaswa wawe na biff halafu wewe katikati yao unakula raha.
😛
 
Mii wasiwasi wangu, wanapokuwa na umoja inakuwa sawa una mke mmoja. Maana hakuna ushindani ambao huongeza ubora. Kwa zamani ingekuwa bomba sana, ila kwa sasa inapaswa wawe na biff halafu wewe katikati yao unakula raha.
😛
Lakini ni bora kuwa na wake wawili wasiojuana kuliko hao pacha
Tatizo mbali na wivu ila hata mwanaume akifanya kosa kubwa kwao watamchangia kwa sababu wapo wawili
Ila tuwaombee maisha mema
Kama nawaona timu ya watoto hapo 😄 🤣
 
Huko Kenya, pacha wawili wamemuomba mwanaume mmoja awaoe ili wasitengane.

Pacha hao wenye miaka 20 wamesema hawataki kutenganishwa hivyo waolewe na mwanaume mmoja.

Bwana Oleman Learat mwenye miaka 26 amekubali kuwaoa Anna na Emily wenye miaka 20 ili tu wasitengane.

Soma mwenyewe hapa chini.

----
Mtangazaji wa redio ya kijamii ya Wambaz ya nchini Kenya, Oleman Learat, mwenye umri wa miaka 26, amepanga kukimbia ukapera kwa kuoa wasichana pacha.

Pacha hao, Anne Samken na Emily Salaon (miaka 20), wameamua kuolewa wote na kijana huyo wakisema hawawezi kutenganishwa, kwa hivyo, wamekubaliana kwamba ni afadhali waolewe na mume mmoja.

“Nimeiambia familia yangu kuhusu nia yangu ya kuwaoa hawa pacha haijakataa lakini wanauliza maswali mengi,” Oleman ameliambia gazeti la Taifa Leo na kuongeza kwamba yeye anaona kama anaoa ‘msichana mmoja’ tu kwani wanafanana kwa kila kitu!

Japo Oleman anasema atawajengea kila mmoja nyumba yake katika boma moja, pacha hao ambao ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha KCA cha jijini Nairobi wamesema itakuwa vigumu wao kukaa mbalimbali.

“Sisi hatujawahi kutenganishwa tangu tukiwa shule ya chekechea,” anaeleza Emily.

“Walimu walitutenganisha kwa mwaka mmoja tukiwa shule ya Sekondari mwaka wa 2021 (wakiamini ndio tutafanya vizuri katika masomo) lakini tuloishi kwa huzuni na upweke sana.”

Oleman anasema alianza uhusiano na warembo hao mwaka jana 2023 na kwamba mwanzo ilikuwa ngumu kuwatofautisha lakini sasa anaweza kuwatofautisha, hasa kwa namna wanavyoongea.

Mwanahabari Oleman amesema alikutana kwa mara ya kwanza na pacha hao katika hafla za burudani na kuvutiwa nao.

“Niliona wanafanana kwa kila kitu. Ukiuliza swali, wanajibu pamoja. Nikaanza kuwachumbia na wakanipenda. Kimsingi huwezi kuongea na mmoja akamtenga mwenzake. Kwa hiyo hata nikipiga simu, lazima niwajumuishe wote wawili,” amesema.

Chanzo: Taifa Leo
Hawajafanana kihivyo.
Pili kwa dini yetu ni haramu kuoa mtu na nduguye.
Lazima yatamkuta tu na hatadumu nao.
 
Hawataki kutengana!!! Hata kitandani wanalala pamoja???
Je, wazazi wameridhia watoto wao wabebe laana ???
Je, muoaji amekubali kuanzisha kizazi cha laana???
Wanaume ni muhimu sana kujiandaa kuwa na kizazi bora kupitia chaguo sahihi la mama bora!
Mwanaume ndiye mwamuzi wa ndoa so upendo wako usizibe au kuzuia uwezo wako wa kufikiri na kuamua kwa hekima.
 
Back
Top Bottom