KENYA: Raila Odinga(NASA) ajitoa kugombea urais wa Kenya uliokuwa ufanyike 26 Oktoba, 2017

Tofautisha kenya na TZ mkuu
Tofauti yake nini?Uchaguzi hautofanyika!Au IEBC itamzawadia Raila ushindi au unadhani kususa kwake kutafanya madai yake yatekelezwe aaa wapi? He has lost a battle before a war!
 
Nilitegemea kupata athari za odinga kujitoa katika uchaguz lakini hujatoa hata moja!
 
Huyu jamaa apimwe mkojo...kama alikuwa hana nia ya dhati ya kugombea kwa nini aliingizie taifa la Kenya hasara ya kurudia uchaguzi? Hopeless NASA
 
Raila ni shujaa na mwamba wa Demokrasia.Historia itamkumbuka tu.
 
Ni njia sahihi kwa mujibu wa katiba ya Kenya hilo ni pigo kwa Uhuru Kinyata sababu muda wa yeye kuitawala Kenya unazidi kuyoyoma na kujiondoa kwa Odinga katika uchaguzi IEBC itawalazimu kuandaa uchaguzi mpya tofauti na huu ambao ulimpa nafuu Uhuru.
 
Sasa Tz tungekuwa na uongozi making na wenye mikakati wangetumia hiyo opportunity, kujijenga zaidi na kukaribisha wawekezaji kwa kujenga mazingira rafiki zaidi, coz ndugu zetu hali yao kwa sasa sio stable, ila kwa sababu huyu Jamaa wetu hajui international politics muache aendelee kupambana na kina Mange Kimambi
 
Ni njia sahihi kwa mujibu wa katiba ya Kenya hilo ni pigo kwa Uhuru Kinyata sababu muda wa yeye kuitawala Kenya unazidi kuyoyoma na kujiondoa kwa Odinga katika uchaguzi IEBC itawalazimu kuandaa uchaguzi mpya tofauti na huu ambao ulimpa nafuu Uhuru.
You are wise.
 
Shocking announcement.
 
Ni njia sahihi kwa mujibu wa katiba ya Kenya hilo ni pigo kwa Uhuru Kinyata sababu muda wa yeye kuitawala Kenya unazidi kuyoyoma na kujiondoa kwa Odinga katika uchaguzi IEBC itawalazimu kuandaa uchaguzi mpya tofauti na huu ambao ulimpa nafuu Uhuru.
Halafu kipindi hicho IEBC wanaandaa uchaguzi Rais atakuwa nani, Odinga au?!

Hebu acha kufikiria kishabiki shabiki.
 
Ni njia sahihi kwa mujibu wa katiba ya Kenya hilo ni pigo kwa Uhuru Kinyata sababu muda wa yeye kuitawala Kenya unazidi kuyoyoma na kujiondoa kwa Odinga katika uchaguzi IEBC itawalazimu kuandaa uchaguzi mpya tofauti na huu ambao ulimpa nafuu Uhuru.

Na huo uchaguzi mpya je ataruhusiwa kuwa mgombea tena kwa mjibu wa katiba?
 
Kwann kasema kesho waandamane nchi nzima ka c mshari huyu.
 
Huyu Odinga ana tapa tapa sana,bora kajiondoa maana wakenya wangepata ugonjwa unaoisumbua Tanzania ugonjwa wa uongozi wa hovyo
 
Kenya haitatawalika tena,

Uhuru atatawala kwa wakikuyu

na wakalenjin tu, naiona kenya

ikipasuka
 
Nilitegemea kupata athari za odinga kujitoa katika uchaguz lakini hujatoa hata moja!
Athari kubwa ni kwamba nchi haitatawalika westen kote

pamoja na coast regions amboko nasa wana wafuasi wengi

watamkataa Uhuru kama raisi wao halali kitakachotokea

wanaweza kujitenga.....lets wait and see
 
Source al Jazeera . Amejitoa baada ya kuona kutakuwa na udanganyifu hivyo UCHAGUZI kuwa incredible. UHURU Kenyata kupitia jubilee atashiriki pasi kujali kujitoa Odinga kupitia NASA. UKANA SHILUNGO.
 
Kama ni kweli nadhani ni uamuzi sahihi,marekebisho yanatakiwa yaanzie kwenye hiki kitu kilichokua designated kinachoitwa 'Tume'.hii tume inatakiwa ikubalike pande zote mbili

Amekubali yaishe salama. Hataki the Hague. Bora Uhuru aapishwe Kenya ibaki salama na yeye astaafu salama. Ushindi ni kwa Wakenya wote wakiwemo Uhuru na Raila. Uamuzi mzuri. Historia aliyoweka inamtosha. Tusisikie tena anarudi. Na walio mashabiki wa siasa wamwache wasimzonge zonge. Nadhani ameshauriwa na jopo lake mahiri la akina Orengo. Huu unaweza kuwa uamuzi bora sana kwa vile hali ilivyo.

Ushauri wetu awasimamie wafuasi wake wasiandamane na wasilete vurugu. Hapo tu. Waache kwa hiari na kwa amani. Tusisikie matairi yanachomwa ama vizuizi barabarani ama nini sijui. Uchaguzi ukifika wakae nyumbani wampe mwenzao Uhuru uongozi. Akishinda wamuungue mkono. Kenya iendelee. Atapata heshima. Hata wenzake wa Jubilee huenda wakamsema sana mwanzoni kwa kuwa atakuwa amewanyima ushindi uwanjani. Lakini baadaye watagundua ameiokoa Kenya.

Alifanya hivi hivi Toivi ja Toivo Namibia. ingawa yeye hakuwa kutoka upinzani lakini angeweza kudai nafasi ya kuongoza Namibia. Makaburu walimwachilia toka gerezani wakidhani itawagombanisha yeye na Mzee Sam Nujoma. Toivo lah! akasema "'wacha' Nujoma agombee aiongoze Namibia." Mazingira yote hayo ni tofauti lakini la msingi ni kukubali kuachia unachodhani una nafasi ya kukingangania kwa ajili ya mustakabali wa taifa lenye watu wengi. Ikiwa Raila hakujua "nini maana ya uamuzi wake", basi tunamwambia toka mbali.

Wamefanya wengi maamuzi ya namna hii kwa jinsi zao. Gandhi alimwachia Jawaharlal Nehru awe Waziri Mkuu India baada ya uhuru 1947.Walipatana tokea 1941 Gandhi akisema Nehru anafaa zaidi kuliko yeye. Hata baba yake Raila, Mzee Oginga Odinga, alimwachia Mzee Jomo Kenyatta atoke gerezani aje atawale ingawa nafasi ilikuwa yake.Wawili hao waliheshimiana sana hadi pale matatizo yalipotokea Kisumu miaka michache baada ya uhuru. Raila mwenyewe alifanya hivi kwa Kibaki akitoa ule usemi wake maarufu: "Kibaki Tosha". Historia ni kama inajirudia vile.

La msingi Raila asimchukie Uhuru wala Jubilee. Wala asitoe kashfa ama maneno chochezi akiwa nje ya ulingo alimokuwemo. Nimelitazama suala la Raila kujitoa kwa namna hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…