Mkuu binafsi sielewi kwa nini Watanzania tunapigia debe train ya umeme ya kutoka Morogoro kuja Dar, tena train yenyewe ni ya kubeba abiria siyo mizigo!! Sometimes priorities zetu ni highly questionable - Mkuu nchi gani Africa yenye umeme wa kuaminka labda Egypt na hivi sasa Ethiopia, hivi sasa nchi zetu hizi haziitaji bullet trains kama Shinkansen za Japan au TGV za Ufaransa - priority zetu ziwekezwe kwenye freight trains siyo passenger trains - mwendo kasi wa kufurahisha abiria auwezi kutufikisha popote - tukumbuke revenue zinakuwa generated kwa kubeba mizigo mingi siyo abiria, abiria ni kama Service tu - actually faida yake ni sawa sawa na hakuna.
Kwa upande wetu mimi ningependelea zaidi kama ujenzi wa reli ya kati wangepewa Wachina kama walivyo fanya wenzetu wa Kenya, haya mambo ya kusema reli yetu tutaijenga in piece meal sielewi mantiki yake hata kidogo - reli inapaswa kujengwa seamlessly na contractor mmoja tangu mwanzo wa reli mpaka mwisho, haya mambo ya kusema kilometer fulani ijengwe nchi fulani zinazo fuata wapewe Taifa lingine, yaani kila contractor anakuja na sleepers zake na reli yake mpaka tufike mwisho sijui tuta engage makandrasi wangapi tena wenye workmanship tofauti ingawa wanasema atakuwepo msimamizi mkuu wa Project hii mimi 'am not convienced hata kidogo, tungekuwa serious tusingezungumzia trains za umeme za abiria kutoka Moro kuja Dar wakati nishati ya umeme nchini bado ni mgogoro, hayo yanaweza kufanyika tukiwa na umeme wa kuaminika hata wenzetu wa Kenya siyo kwamba wanashindwa kuweka Loco za umeme wanasubiri mpaka watakapo kuwa na umeme wa kutosha na kuaminika - Locos ni rahisi kuzibadirisha kutoka kwenye mfumo wa Diesel Electric to pure Electric Locos at opportune time siyo hivi sasa.