Kenya: Serikali yatangaza kuwepo kwa njaa

Kenya: Serikali yatangaza kuwepo kwa njaa

Kwetu hapa hakuna njaa....
Kweli hakuna njaa wala dalili ya njaa bali kuna ukame kiasi na upungufu wa nafaka ya mahindi peke yake mchele ifakara wanalia soko huko mihogo imejaa mtama umejaa viazi vitamu na mbatata vimejaa karanga zimejaa njaa inaingilia wapi?
 
Yaani mkuu huwa najiuliza sana hawa wanao mtetea kwa haya afanyayo sasa ni kutawaliwa na ujinga au upoyoyo?
Maana kama ni Watanzania wanadharau mambo mazito hivi kwa wananchi utadhani ndugu na jamaa zao wote wanaishi New York kumbe wako huko Nanjilinji na shida na mashaka matupu.
Jee hawana huruma na ndugu hata kama wao wana maisha mazuri?
Huruma ya nini kwani ikitangazwa njaa ndio itasaidia nini? Sasa kwa taarifa yako huko ulikotaja kuna mihogo kibao
 
Kwa Kenya kuwa na uhaba wa chakula ni suala la kawaida, watz tunapenda sana siasa mufilisi. Tz ni mvua ni mvua za vuli zimechelewa au zimegoma baadhi ya sehemu, tuna hatari ya baa la njaa na sio tuna baa la njaa. Kama mvua zingenyesha ktk hali ya kawaida bado mazao yangekuwa shambani hadi leo inashangaza mtu kulia njaa saivi.
tuko vizuri tuna upungufu wa mahindi tu lkn vyakula vingine kibao. Ifakara wanalalamika hawana soko la mchele njaa gani hiyo?
 
Kweli hakuna njaa wala dalili ya njaa bali kuna ukame kiasi na upungufu wa nafaka ya mahindi peke yake mchele ifakara wanalia soko huko mihogo imejaa mtama umejaa viazi vitamu na mbatata vimejaa karanga zimejaa njaa inaingilia wapi?
Anchosema bwana mkuubwa ni sawa..
 
Naomba kuchangia kwenye mada hii..

Kwa kweli kuna maeneo mbalimbali nchini Kenya ambako mvua huwa hainyeshi kwa muda mrefu sana, kama vile pande za Nothern Kenya. Ni sehemu kubwa sana, karibu nusu ya ardhi ya nchi.

Kwenu Tanzania naona hamna shida ya mvua sana kama hapa kwetu. Mna nafasi nzuri sana ya kuwa na chakula cha kutosha ikiwa kutawekwa mikakati inayostahili.
 
Salama wa kuu....

Nipo naangalia NTV, Serkali ya Kenya inatangaza kuwepo kwa ukame na upungufu wa chakula katika eneo kubwa la nchi. Inatoa takwimu muhimu juu ya chakula kilichopo na jitihada za serkali kutatua tatizo.

............
BADO KWETU
Kichwa cha habari ni tofauti na habari
Ukame ni tofauti na baa la njaa
 
Back
Top Bottom