MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Na TPDF inapoenda kulinda amani huwa inaletewa ripoti nzuri daily sio utani.
Ila sioni Hilo kwa KDF.
Hamna sehemu nimeibeza TPDF, ni taasisi yenye heshima zake na historia, ila nimesema hawajakumbana na changamoto za adui wa kisasa, adui wa leo ameshinda hata majeshi ya Marekani ambao uwezo wao ni mara elfu ya TPDF. Huyu adui wa leo hapigani vita rasmi, ni mfia dini aliyelishwa mambo ya kidini kiasi cha kuwa zombi, anaishi ndani ya jamii na kufanya kila kitu cha kawaida, kuvaa kanzu na kuonekana kama mpenda amani na mcha Mungu, ila ndani ya akili zake anajijua mwenyewe.
Tumekua na matukio ya wafia dini wa kutokea Tanzania ambao pia wamehusika kwenye baadhi ya mashambulizi huku, hiyo inafaa ikuingie ni aina gani ya vita tunavyopigana.
Mambo ya kwenda kulinda amani sio kitu cha kutambia maana pia KDF wamefanya tu sana.