Kenya vs Tanzania: Mbona Kuna Chuki?

Elly Owange

Member
Joined
Jun 2, 2012
Posts
11
Reaction score
36
Mimi ni mkenya, na nimejiunga na hii forum kwa sababu hivi karibuni nitahamia kuishi TZ kwa miezi 5 hivi. Ila nimehuzunishwa na ushindani kati ya +255 na +254 niliouona hapa. Nina swali kwa ndugu zangu waTZ, mbona mnachuki dhidi ya Kenya hivi? Hii sehemu inaitwa; Kenya News and Politics. Ila mada zilizojaa hapa nyingi ni za kuonesha maendeleo ya Tanzania (ili kuonyesha mko juu ya kenya) na mada za kuiponda Kenya tu.

Explain to me what you gain from comparing the two countries? Kama mnaona Tanzania imeshinda Kenya kimaendeleo, mbona poa tu! Mbona hamjilinganishi na UG, RW ama Malawi? Kenya tu ndio wayaumisha kichwa! Ina inawafaidi nini kuiponda Kenya? Mnafurahia Kenya ikianguka ama ni vipi? Mara ooh SGR haitafika malaba, mara ohh tumewapokonya pipeline ya UG, RW SGR itapitia Tz, mara ohh lapset project itaanguka! Mara ohh wakenya wanaishi kwa slums, mnasahau dar ina Mbagala na tandale slums. Hata S.A most developed country in Africa ina slum; Soweto.

Mimi sina kinyongo nikiona Tz ikiendelea, na wakenya wenzangu 40 million hakuna atakaepandwa na presha Tz ikipita kenya. Sasa mbona nyinyi inaonekana ni kama mnataka Kenya ianguke. Sijui neno la kiswahili ila wazungu watasema you have inferiority complex. Tembeleeni Forums za Kenya kama; JamiiForums.com, Wazua Forum. Hutaona hata mada moja inayoongelea TZ. Hata hakuna sehemu ya "Tanzania News and Politics

Nchi EAC zina watu jumla zaidi 170 million, tukiungana kufanya biashara na maendeleo itafaidi Nchi zote tufike kiwango cha Nigeria, SA na Egypt. Ila waTz nyie mnaona kushindana na kenya tu. Niambieni mnafadi nini kulinganisha Kenya na Tz, wakati hata kenya hatujali?

Kwa hayo mengi nangoja kwa hamu kuja TZ.

Poleni kwa waliopata wakati mgumu kuelewa kiswahili changu.
 
Unahangaika wakenya ambao hata hiyo nchi tunaweza kufanya koloni letu pambafu kabisa hamjui kipindi cha ukoloni tz ikukuwaga mashamba na wakoloni wakimaliza kulima wanakuja kenya kutumia pesa williamson muanzili wa mwadui alikuwaga anakuja kunywa tea kwa ndege nairobi anarudi kuchimba hamuoni aibu kushindana na kushidwa na manamba wenu kipindi cha ukoloni
 

Elly Owange
unamuona huyo hapo. sasa yeye hapo anafaidika na nini? na unamshauri nini?
 
Hii si chuki aisee hizi ni stimu za wanzuki. Fika hapo nje ule samosa tano, hela ntakutilia kwenye M-pesa! 😀
 
Tanzania nimepaishi miaka kadhaa, na nimekatiza mikoa mingi na wilaya nyingi, nimeingia maeneo mengi sana huko na kuhititmisha kwamba kuna aina tofauti tofauti za Watanzania.
- Kunao ambao walikaririshwa mambo fulani fulani dhidi ya Wakenya tangu enzi za ujamaa, hawa hata ufungue nyuzi ngapi humu hawatabadilisha mawazo na mitazamo yao, ni wazee wazee na cha kuhuzunisha walipokeza mitazamo ya kihivyo kwa watoto wao. Hawa walikaririshwa kwamba Kenya ilijengwa na mzungu na ndio sababu imewashinda kiuchumi hadi leo.

- Kuna wale japo huiskia Kenya, lakini ukimuuliza iko upande gani kwenye ramani hawana habari, hawa hujifanya wajuzi sana wa masuala ya Kenya, na wapo hata humu JF. Sampuli ya hawa utawakuta vijiweni Tanzania wakiijadili Kenya, nilikua nakaa pembeni kuwaskliza hadi naishia kicheko.

- Kuna ambao kwa kweli wanaipenda Kenya, hawa aidha wamewahi kuishi na kusomea Kenya maana kila nikijadili nao walikua wanaonekana kuwa na habari za Kenya hadi za hivi punde. Unakuta Mtanzania anawajua wabunge wetu hata kunizidi, anaweza akaongea siasa za maeneo kama Nyandarua, Trans Nzoia n.k. yaani maeneo ambayo hata mimi binafsi sina habari nini kinaendelea huko, wa hivi nilikua na urafiki nao sana na mpaka leo huwa tunapigiana simu.

- Kuna wengine japo wamewahi kuishi Kenya, lakini kuna kituko kiliwatendekea wakaishia kulea chuki dhidi ya Kenya, aidha alinyang'anywa bidhaa, au kiwanja au fursa fulani, kuanzia hapo akaanza kuishi full majungu na machungu dhidi ya Kenya, na wapo humu.

- Kuna sampuli ya wengine ambao walizembea kazini kwao huko halafu Wakenya wakaalikwa na kuajiriwa kwenye hizo nafasi, unakuta mwajiri Mtanzania ameamua kumlipia Mkenya au Mhindi gharama zote za usafiri, makazi, vibali vyote ilihali ameacha Watanzania wenzake. Sasa hapa jamaa wanaishia kulea chuki na hawawezi kubadilika hata ufanye nini.

- Kuna wengine ambao hutuchukia kwa ajili ya uwezo wetu wa kuongea kingereza ilhali wao wamehangaika kwa muda mrefu, unakuta tukiingia vikao ambavyo kingereza ndicho kinatumika, inakua rahisi kuwajua Wakenya humo ndani maana wanaonekana kujiamini na waongeaji ilhali Watanzania kimyaaa. Vikao vya namna hii nilivihudhuria sana, Watanzania walikua wanalea chuki japo kimya kimya.

- Lakini pia humu JF kuna wale ambao ni mamluki wa CCM, hawa hukesha humu wakiponda Kenya, wao hawana chuki lakini wapo kikazi zaidi. Awali nilikua najadili nao lakini nilipogundua kwamba ni kama robots, yaani kazi yake haimruhusu kuwa na mtazamo tofauti, hivyo hata kama uko sahihi kivipi hatokubali hata kama uzi utaishia kwenye kurasa ishirini, ikabidi niwe nawakwepa.

Zaidi ya yote, kuna Watanzania wazuri tu, mnahusiana nao vizuri hawana chuki wala nini, tena wachapa kazi nimefanya nao kazi, wana uzalendo wa Kiafrika, yaani wao hupenda kuona maendeleo kwenye nchi yoyote ya Afrika. Na hutawakuta wakichangia kwa chuki, wao hutoa hongera wanapokumbana na hatua zozote chanya zitakazoikomba Afrika kiuchumi. Wapo wa hivi humu lakini wachache sana.
 
hizi bots zimejaa sana hapa kwa Kenyan Section. kumbe ziko kwa payroll?! kazi zao haziwaruhusu ziwe na mtazamo mmoja na Wakenya.
 
Acheni kulialia hapa JF, Wakenya mnaadika kama vile nyinyi ni watakaifu. Hakuna cha utakatifu wala nini, ukweli ni kwamba wakenya hampendi kushirikina na wenzenu kama hakuna pesa mbele. Hakuna hata siku moja utasikia msemo huu kutoka kwa Mkenya "kizuri kula na ndugu yako", wengi wenu mnatuambia kila mara Kenya haina undugu kwenye biashara, haya sasa, Uganda, Rwanda, Tanzania Buruindi S.Sudan wanajivuta pembeni mpaka mjielewe kama majirani zenu wana thamani kubwa kwenye ustawi wenu.
 
Sina cha kuongeza, Kenya inabidi ichague kushirikiana na USA au kushikamana na nchi zingine za EA, Kagame, Mseven na Magufuli walishasema hawatotushwa na vitisho vya Marekani katika hili, at least Kagame na uncle Magu ninawajua wakisema wamesema, hata uwachinje hawawezi kubadilika, tutaona mwisho wa Kenya katika hili.
 
Tujitaarishe kuwaweka pembeni, jaama wanavyo penda pesa hawawezi kuachia $500million ya AGOA iwatoke. Angalia walivyo shidwa kukubalina na wezao kwenye EPA, wakenya tunawajuwa ikija kwenye maamuzi magumu kati ya utu na pesa.
 
Watz ndvo tulivo asee! Ukiona hvo mjue kenya mwatuzidi hence. Watu wanashndwa kuulizwa wat is ur secret instead wanataka kujiaminisha uongo? Hii ipo JF ht kwa tz na tz hasa kwa makabila?utakuta mtu analazimisha kabila lao lina kila kitu huku akijua wanaoongoza kwa sekta fulan ni akna nan?ili tu ajiaminishe kwamba wapo hivo kumbe si kweli?
 
Ww hapo umewaona watz tuu wakenya hujawaonaa vilee wanaongea ropo ropoo..
 
Nyie ndio mliotuanza na vizabinazabina vyenu mmelikoroga lazima mlinywe babu weye sisi wala hatukua na Tatizo na nyie matatizo mmeyaleta wenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…