Tanzania nimepaishi miaka kadhaa, na nimekatiza mikoa mingi na wilaya nyingi, nimeingia maeneo mengi sana huko na kuhititmisha kwamba kuna aina tofauti tofauti za Watanzania.
- Kunao ambao walikaririshwa mambo fulani fulani dhidi ya Wakenya tangu enzi za ujamaa, hawa hata ufungue nyuzi ngapi humu hawatabadilisha mawazo na mitazamo yao, ni wazee wazee na cha kuhuzunisha walipokeza mitazamo ya kihivyo kwa watoto wao. Hawa walikaririshwa kwamba Kenya ilijengwa na mzungu na ndio sababu imewashinda kiuchumi hadi leo.
- Kuna wale japo huiskia Kenya, lakini ukimuuliza iko upande gani kwenye ramani hawana habari, hawa hujifanya wajuzi sana wa masuala ya Kenya, na wapo hata humu JF. Sampuli ya hawa utawakuta vijiweni Tanzania wakiijadili Kenya, nilikua nakaa pembeni kuwaskliza hadi naishia kicheko.
- Kuna ambao kwa kweli wanaipenda Kenya, hawa aidha wamewahi kuishi na kusomea Kenya maana kila nikijadili nao walikua wanaonekana kuwa na habari za Kenya hadi za hivi punde. Unakuta Mtanzania anawajua wabunge wetu hata kunizidi, anaweza akaongea siasa za maeneo kama Nyandarua, Trans Nzoia n.k. yaani maeneo ambayo hata mimi binafsi sina habari nini kinaendelea huko, wa hivi nilikua na urafiki nao sana na mpaka leo huwa tunapigiana simu.
- Kuna wengine japo wamewahi kuishi Kenya, lakini kuna kituko kiliwatendekea wakaishia kulea chuki dhidi ya Kenya, aidha alinyang'anywa bidhaa, au kiwanja au fursa fulani, kuanzia hapo akaanza kuishi full majungu na machungu dhidi ya Kenya, na wapo humu.
- Kuna sampuli ya wengine ambao walizembea kazini kwao huko halafu Wakenya wakaalikwa na kuajiriwa kwenye hizo nafasi, unakuta mwajiri Mtanzania ameamua kumlipia Mkenya au Mhindi gharama zote za usafiri, makazi, vibali vyote ilihali ameacha Watanzania wenzake. Sasa hapa jamaa wanaishia kulea chuki na hawawezi kubadilika hata ufanye nini.
- Kuna wengine ambao hutuchukia kwa ajili ya uwezo wetu wa kuongea kingereza ilhali wao wamehangaika kwa muda mrefu, unakuta tukiingia vikao ambavyo kingereza ndicho kinatumika, inakua rahisi kuwajua Wakenya humo ndani maana wanaonekana kujiamini na waongeaji ilhali Watanzania kimyaaa. Vikao vya namna hii nilivihudhuria sana, Watanzania walikua wanalea chuki japo kimya kimya.
- Lakini pia humu JF kuna wale ambao ni mamluki wa CCM, hawa hukesha humu wakiponda Kenya, wao hawana chuki lakini wapo kikazi zaidi. Awali nilikua najadili nao lakini nilipogundua kwamba ni kama robots, yaani kazi yake haimruhusu kuwa na mtazamo tofauti, hivyo hata kama uko sahihi kivipi hatokubali hata kama uzi utaishia kwenye kurasa ishirini, ikabidi niwe nawakwepa.
Zaidi ya yote, kuna Watanzania wazuri tu, mnahusiana nao vizuri hawana chuki wala nini, tena wachapa kazi nimefanya nao kazi, wana uzalendo wa Kiafrika, yaani wao hupenda kuona maendeleo kwenye nchi yoyote ya Afrika. Na hutawakuta wakichangia kwa chuki, wao hutoa hongera wanapokumbana na hatua zozote chanya zitakazoikomba Afrika kiuchumi. Wapo wa hivi humu lakini wachache sana.