Kitu cha kwanza, ni chema chajiuza, kibaya chajitembeza, hivyo kama muziki wako ni mzuri, utajiuza.
- Hatua ya kwanza baada ya kurekodi single yako, na video yake, fungua account yako kwenye mitandao ya kijamii, facebook, instagram, tictoc, X, linkediln, whatsapp, na youtube hivyo nyimbo yako kuanza kuonekana kwa kuituma hiyo single yako watu waanze kuisikiliza. Anza kwa kuwatumia watu wote wanaokujua. Kujiunga na mitandao yote ni bure!.
- Hatua ya pili, ni kuisambaza kwenye vituo vya TV, redio na magazetini, kwa wewe kuiweka kwenye flash na kuipeleka mwenyewe physically, kote utapokelewa, wataipokea single yako na kuisikiliza, baadhi ya Watangazaji watakudodosa, unatuachaje, wakitegemea utoe chochote ili na wao wa kupromote, waambie ukweli, kama una kidogo kitu, wapooze, kama huna kitu kabisa, waeleze wazi wewe ni upcoming ndio unaanza na huna kitu. Wimbo wako wataucheza tuu hata bila kutoa chochote na kama ni mzuri, uta hit tuu, Mondi alianza na Nenda Kamwambie akaja na Mbagala, akatoka.
- Ukianza kuwika, social media media zako zikapata views za kutosha, tafuta pesa kidogo, kama laki, laki mbili, lipia social media promoter ili kuboost social media page zako, ili kuingia kwenye monetisation, uanze kulipwa kwa social media.
- Kama wimbo wako ni mzuri, utaanza kupata mialiko ya kufanya shows, utaanza kulipwa, na mwisho wasanii wakubwa watakuona na kukupa mikataba ya kujiunga na record lable zao.
- Mambo yakianza kuchanganyia, maokoto yakaanza kuonekana, then ajiri meneja atakusaidia kukupaisha, utkuwa umeisha toka.
Mimi eneo langu la specialization sio kwenye promotion, mimi ni producer wa vipindi vya TV,Redio, Magazeti na online media, ambaye nawasaidia wenye vipaji vya utangazaji kujiajiri.
https://www.jamiiforums.com/threads...i-na-utangazaji-vipindi-vyako-vya-tv.1206955/
P