Kenya wagonjwa wa Coronavirus waongezeka na kufikia 15. Mipaka yafungwa

Kenya wagonjwa wa Coronavirus waongezeka na kufikia 15. Mipaka yafungwa

Kwa mengi tu, kuanzia utoaji huduma za kiafya, mazingira tunayoishi + umasikini.

Kwa mfano hali ikiwa mbaya raia tukalazimika tujifungie majumbani kama ilivyo Italy kwa sasa unafikiri wata survive wangapi?
 
Nilikua naangalia aljazeera asubuhi hii nimeona WHO wanaitahadharisha Africa ijiandae na hali mbaya

Wala sishangazwi na maoni ya WHO, kama tutapuuzia suala la kusitisha walao kwa mwezi mmoja/miwili masuala ya waumini kuhudhulia ibada makanisani na misikitini na kupunguza idadi ya wasafiri wanao tumia mabasi mjini basi ugonjwa huu utaenea kwa kasi na tutashindwa kudhibiti kwa kukosa nyezo za kuhudumia kila mgonjwa - kasi ya kuenea ugonjwa huu inatisha sana - na sisi tuanzishe kikosi cha kupulizia dawa mara kwa mara kwenye mkusanyiko mwingi wa watu na majumbani kama walivyo fanya wenzetu Wachina na Warusi na wajafanikiwa pamoja na juhudi nyingine za ziada.

Kwa nini nasisitiza upulizaji wa dawa, nimeona jana Warusi na Wachina walipeleka malori ya kupuliza dawa huko Italy walipeleka vile vile waganga na wana taaluma ya magojwa yanayo sababishwa na virusi - swali ni: kwa nini magari ya kupulizia madawa wanayapa kipa umbele zaidi - kuna litu walicho jifunza si bure - na sisi tuwaige kabla hatujachelewa watupatie formula ya dawa wanazo tumia kupulizia naona mbinu hii hiko effective kweli kweli.
 
Bukyanagandi,
Kabla huo ugonjwa kuenea kwa kasi Afrika nategemea wazungu watakua wamegunduaa dawa, maana tutakufa sana kama kuku.
 
Asilimia 95 ya wafanyakazi wa safaricom kampuni ya simu kenya wanafanya kazi kutoka majumbani mwao. Vyuo na mashule vimeandaa masomo kupitia mitandao na vipindi maalum vya radio.

In Kenya, Safaricom and Nation Media Group said they had acquired and were providing laptops, dongles and tech tools to their employees. Safaricom said over 95 per cent of its workforce has been asked to work from home.

Microsoft announced that it is offering its Microsoft Teams collaboration platform, for free, to companies to make remote working possible.
 
Kabla huo ugonjwa kuenea kwa kasi Afrika nategemea wazungu watakua wamegunduaa dawa, maana tutakufa sana kama kuku.

MK254, asubuhi hii nilikuwa nazungumxa na ndugu yangu huko Ujerumani - anasema yaani watu wana chukua tahadhali kubwa hata majirani hawatembeleani, misikiti na makanisa yamefungwa na masuala ya sherehe starehe na mkusanyiko wa watu zaifi ya wanne vinepigwa marufuku hisipo kuwa wanafamilia ndio wanaruhusiwa kuishi kwenye nyumba moja.

Kinacho nishangaza mimi kwa nini Serikali zetu Africa Mashariki zinapuizia ukweli huu ambao unawrza kuinusuru Africa - Corona si lele mama - tusipo kuwa makini utabiri wa Bill Gates unaweza kuangamiza watu wengi chini ya sub sahara Africa. Gooday MK254.
 
Nawaona Ulaya, maana kule Quora wanatupia mapicha na taarifa za maisha yalivyo, wao wamechukua tahadhari na kufuata maagizo.

Hapa Afrika huwa tupo tupo tu ilmradi siku zinaenda, naibu gavana kwetu hapa Kenya kiongozi mzima mwenye akili zake ametokea Ujerumani na kutinga kwake nyumbani, mpumbavu amewaponza familia yake yote, halafu lilivyo lijinga liliingia maeneo ya burudani na kula bata miongoni mwa wateja wengine wote, limefanya vikao kote kote yaani tumekaa mkao wa kuskliza maana sijui itakua vipi.

Hapa hata sijui kama ni kuomba Mungu tutatumia mbinu gani labda.
Anyway good day.
 
Bukyanagandi, Ninajaribu sana kufuatilia huu mjadala wa Nyumba za ibada kwa undani sana lakini ni nashindwa kupata jibu, sijui nianzie mguu gani kuingia. Ila jambo moja ninaloweza kusema "Sisi waafrika na watu wote duniani wenye kuamini uwezo na uwepo wa Mungu ni hovyo kabisa, hatuna akili na hatupaswi kusikilizwa hapa duniani hata kidogo.

Vipi leo tunamkimbia MUNGU, hatutaki hata kukaribia nyumba zake?. Sisi huwa mstari wa Pele kuwasema wazungu kwamba wamepotea kwa kufanya mambo aliyokataza Mungu, Kama vile ndoa za jinsia moja, lakini sasa hivi sisi tunaompenda huyo MUNGU ndio tunaongoza kumlaani mtu anayetuambia tufuate amri kuu ya Mungu ya kuenda katika nyumba za ibada, badala yake tunahimizana kutokwenda kwamba ndio jambo la busara.

Hivi yale maneno tunayoambiwa na viongozi wa dini kwamba Mungu ndio kimbilio letu, yeye hashindwi na lolote lile, tumeisahau sasa hivi tunahisi Corona ni zaidi ya Mungu?

Mimi najaribu kuwaza peke yangu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wataalam wa probability na logarithm wanaweza kukisia ongezeko la wagonjwa.
 
Breaking news Kenya idadi ya wagonjwa wa coronavirus imeongezeka hadi 25.
Screenshot 2020-03-24 at 4.17.33 PM.png
 
Breaking news Kenya idadi ya wagonjwa wa coronavirus imeongezeka hadi 25.View attachment 1398126

Naiona lockdown inatua hapa, maana hao waliogunduliwa kila mmoja ameambukiza huko na walioambukizwa wameambukiza kule waliko....mwendo wa kuambukiza halafu ndugu zangu Wakenya nawaona wengi hatupo serious, hatuachi upumbavu wetu wa kukusanyika makundi au kuwazingira wanasiasa, tutaambukizana hiki kidude hadi tutie akili.

Ona hii picha hapa jamaa wamemzingira gavana Anyang Nyongo, hawaonekani kujali au kuchukua tahadhari ya kukaa mbali na umati wa watu.

Nimeona sehemu hata Tanzania nako ndio usipime, watu wamemzingira Makonda huku akitema cheche dhidi ya Mbowe na Zito Kabwe halafu umati unamshabikia kweli.

MAINPIC.jpg
 
MK254,
Ukaidi mwingi,mfano baada ya bar kufungwa watu wamehamia kweye busaa and changaa dens! Leo hii gavana Mandago alikuwa na kazi ya ziada kuwatimua kwenye machimbo ya pombe haramu. Kazi kwelikweli.
 
Mimi najiuliza maswal kilacku cpati majibu ,hv Kuna aliesikia taarifa zozote za korona kuhusu Urusi a.k.a Russia

Sent using Jamii Forums mobile app

Warusi wapo 146million lakini kesi za Corona ni chache kuliko hata Luxenberg
Hili ni kwa sababu wao walifunga mpaka wa na China ambao ni maili 2600 tangu mwezi wa kwanza
Hawakusubiri chochote bali putin aliamua haraka mipaka ifungwe na hiyo ndio sababu ya kupambana nao

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Ukaidi mwingi,mfano baada ya bar kufungwa watu wamehamia kweye busaa and changaa dens! Leo hii gavana Mandago alikuwa na kazi ya ziada kuwatimua kwenye machimbo ya pombe haramu. Kazi kwelikweli.

Asubuhi nimepitia sehemu nikakuta bar inafunguliwa mlango walevi waondoke maana wamekesha humo wakinywa kimya kimya, subri labda tukianza kufa kadhaa ndio majitu yatazinduka.
 
Nchi zote duniani zina watu wajingawajinga.... Ila wengi wao wapo bara letu hili.
 
Asubuhi nimepitia sehemu nikakuta bar inafunguliwa mlango walevi waondoke maana wamekesha humo wakinywa kimya kimya, subri labda tukianza kufa kadhaa ndio majitu yatazinduka.
Pamoja na kusikitisha mengine hadi kichekesho.
 
Back
Top Bottom