NCHI ZA KIAFRIKA ZINAZOONGOZA KWA KUWA NA SATTELITE NYINGI NDANI YA AFRICA.
Hizi Rank zilitolewa na SpaceHubs Africa mnamo tarehe 19/08/2024. Spacehubs Africa walitoa list hiyo siku hiyo ukizingatia siku tatu nyuma yani tarehe 16/08/2024 ndio ilikuwa siku ambayo nchi ya SENEGAL ndio ilikuwa nchi latest(nchi ya mwisho hivi karibuni) kulaunch Sattelite yao ya kwanza tangu kuwepo kwa Taifa hilo huko juu kwenye space ambayo waliita GAINDESAT-1A.
Mpaka kufikia taarifa hizi zinachapishwa tarehe na mwaka huo, ni takribani Sattelite 61 zimesharushwa kutoka kwa nchi za Kiafrika 17. And also 10 of those 52 sattelites were launched by Commercial Entities.
Katika hizi Rank, kushoto ni namba, itafuata Nchi na idadi ya Sattelite walizo launch kwenda kulia. Tuanze.
01. South Africa - 13
02. Egypt - 13
03. Nigeria - 7
04. Algeria - 6
05. Morocco - 3
06. Kenya - 3
07. Angola - 2
08. Ethiopia - 2
09. Rwanda - 2
10. Djibout - 1
11. Ghana - 1
12. Mauritius - 1
13. Senegal - 1
14. Sudan - 1
15. Tunisia - 1
16. Uganda - 1
17. Zimbabwe - 1
Extra: Pan-African - 2
Source: SPACEHUBS AFRICA
Website: spacehubs.africa
Link:
List of African countries with satellites — SPACEHUBS AFRICA
Na hizo nchi zina Mashirika yake ya ndani ya Nchi zao ya kudeal na anga(Space Agency) na mengine wamechanganya anga na Sayansi kwa ujumla.
Zipo Space Agency Kongwe zilizoanzishwa tangu 90's na Nchi zingine ziliamua kubadilisha majina ya Space agency zao. Zipo tarehe rasmi zinazoonyesha zilianzishwa mwaka gani na gani.
Sisi Tz bado hata hiyo Space Agency tangu tupate uhuru mwaka 61 hata hatujaianzisha hadi sasa itakayodeal na Maswala ya Anga.
Aidha mnamo tarehe 18/05/2023 Rais Mama Samia Suluhu Hassan alisema Tanzania ina mpango wa kusuka Sattelite yake na kuirusha pia kuanzisha Space Agency yake. Pia mwaka huo huo 2023 tulimsikia Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia Mhe. Nape Nnauye(Mb) akisema ya kuwa Serikali imeazimia kuanzisha Shirika lake la Anga la Tanzania(Space Agency) kwa mwaka 2023,2024 au 2025 ili na sisi tuweze kurusha Sattelite. Ndio tunaendelea kusubiri, Ukizingatia sasa hivi Nape hayupo katika hiyo Wizara kwani ametenguliwa.
Angalia
View: https://youtu.be/c1MWeQd88WQ?si=1bph4SfO0EfE80e8
Pia tazama
View: https://youtu.be/20LWjJuLLZ8?si=qIE5oZAVNlJmebsf
Mnamo miaka ya 1970's na 1990's katika zile vita baridi kati ya Umoja wa Kisovieti(USSR) na USA, miongoni mwa vitu walivyokuwa wakitambiana na kushindana ni kwenye mambo ya Anga pia. Walikuwa wakishindana kwenda kweny Space na kwenye mwezi pia.
Katika kipindi hicho nchi nyingi za Africa zilikuwa hazifungamani na upande wowote ule na pia zilikuwepo nchi chache zilizojipambanua kwa kuchagua upande either USA au USSR.
Katika kipindi hicho Nchi kadhaa za Africa zikaweka ndoto na wao waanzishe Space Agency zao hata kama walikuwa hawana Teknolojia kubwa. Sasa sijui sisi Tz tulikuwa tumelala wapi katika kipindi hicho, ukizingatia nNchi nyingi za Kiafrika hali zetu za Uchumi GDP zinafanana tu. Ukweli ni kwamba katika anga Tz bado tuko nyuma, ila tutakuja tu kua mbele iko siku.
Ila ninaiombea Nchi yangu Tanzania tufike tunapopakusudia katika hizi medani za Anga na Kwa uweza wa Mungu tutafika huko. Amen.