Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Bila shaka watu wote tumeona namna vijana wa Kenya maarufu kama generation Z walivyoitisha mtiti mzito kwa kupiga maandamano mazito mitaani ya kupinga mswada wa bajeti uliolenga kuwakamua zaidi kupitia kodi na tozo mbalimbali. Vijana wale kupitia mitandao ya kijamii pasipo msukumo wa wanasiasa wameweza kuhamasishana na kujipanga vyema, wamepiga kunji zito mtaani pasipo kujali vitisho, risasi, maji ya kuwasha, mabomu ya machozi, virungu vya mamia ya polisi katili wa Kenya waliomwagwa mitaani kuwadhibiti. Hamasa na mtindo wao wa kupiga maandamano umekuwa wa kipekee mnoo kiasi cha kuitisha serikali ya Kenya na kuiamsha dunia.
Huo ndio upande wa vijana wa Kenya, ukija upande wa Tanzania, upande wenye vijana watumiaji wengi zaidi wa mitandao huenda kuliko nchi yoyote ile katika ukanda wa Afrika mashariki na kati, vijana wake wako busy mnoo mitandaoni kusaka connection za ngono na umbeya, kubet, kuchambua soka, kupost picha zao zilizohaririwa, kudanga na kusaka madanga na kubwa kuliko yote kuupigia debe uchawa.
Leo hii hapa Tanzania, vijana machawa ndio kizazi cha dhahabu, machawa wanapewa mpaka mialiko rasmi bungeni na Ikulu. Uchawa umepewa hadhi ya kipekee, vijana wanajivunia uchawa, vijana wanatamani kuwa machawa na serikali inaupigia debe uchawa kama ndio njia bora ya kujiajiri.
Maskini vijana wa Tanzania!