Kenya: Wanaume waandaa mgomo

Kenya: Wanaume waandaa mgomo

...wiki hii tangu imeanza masikio yangu yamekua yakikutana na habari za
wanaume wa nchini kenya katika mkoa nisioukumbuka jina,
wanakula mkong'oto wakutosha kutoka kwa wake zao..
na hao vidume wakenya wamekuaje tena banaaa!!
naogopa mm maana ikitapakaa ikija tz nomaaaaaaa!!
 
......mwanamke akikusumbua mpige m i m b a - Ephraim Kibonde kupitia Jahazi lake
 
...wiki hii tangu imeanza masikio yangu yamekua yakikutana na habari za
wanaume wa nchini kenya katika mkoa nisioukumbuka jina,
wanakula mkong'oto wakutosha kutoka kwa wake zao..
na hao vidume wakenya wamekuaje tena banaaa!!
naogopa mm maana ikitapakaa ikija tz nomaaaaaaa!!

Strength of women!
 
Endeleeni na mambo yenu ya women empowerment mtaona after ten years! Mbona hapa bongo midume kibao imekaa kizembezembe kama mdada, mwanaume anatengeza kucha, anasuguliwa miguu, scrub, shit sana.
Hivi mwanaume kama huyo hata mlango ukibomoka hawezi kushika nyundo na kugonga msumari.
Gari imepata pancha eti hawezi kupiga spana mpaka ampe mtu buku mbili afungue tyre!
Kwa nini mwanamke wako asikudunde mwanaume suruali mkubwa we!
 
Equality for all.
 
Na wapa big up wanawake wakenya,
Maana wanakomesha ukatiri wa wanaume kwa wanawake na watoto
Twende kazi wakenya na waTZ wakiiga mbona itakuwa mwake, maana kunajirani yangu hapa kila akirudi amelewa lazma
amtandike mkewe na watoto
 
[TABLE="width: 491"]
[TR="bgcolor: #E1E1E1"]
[TD]
6267930.jpg

Mwenyekiti wa chama cha wanaume akimpa pole mwanamume aliyepigwa na mkewe[/TD]
[TD]
Kenya, wanaume wanapanga kugomea vyakula vya wake zao kwa siku sita kutoka na kuongezeka kwa visa vya wanawake kuwapiga waume zao. Kwa hiyo badala yake wanaume watakuwa wakila kwa mama ntilie.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 3"]Taarifa kutoka Nairobi Kenya, Zilizonukuliwa na mashirika ya habari zinaripoti kuwa Mwenyekiti wa Chama cha maendeleo ya Kina baba Nderitu Njoka amesema mgomo huo wa siku sita una lengo la kuwashinikiza wanawake kukoma kuwanyanyasa na kuwapiga waume zao.
Kiongozi huyo Nderitu Njoka amesema kuanzia leo jumatatu ataanza kampeni ya kuwashawishi akinababa kula mahotelini badala ya majumbani mwao. Mwenyekiti huyo wa maendeleo ya wauaume alikuwa akizungumza katika hospitali kuu ya mjini Nakuru huko Rift valley ambako alikuwa amekwenda kumliwaza baba mmoja ambaye amelezwa humo kutokana na kipigo alichopewa na mkewe.

Baba huyo akizungumza kwa uchungu hospitalini alisema mkewe alimuita nyumbani akachukuwe pesa kabla ya kumfungia chumbani na kumtandika. Kwa muujibu wa bwana Nderitu Njoka, mkoa wa kati nchini Kenya ndio unaongoza kwa idadi ya akina baba wanaopigwa na bibi zao.

Katika mkoa huo wa kati wanaume karibu nusu milioni wameripoti kutandikwa. Chama hicho cha wanaume kimedai kuwa kuna wanaume ambao wanalazimishwa kufuo nguo za wake zao. Wengine pia wamedai kunyimwa tendo la ngono na mabibi zao.

Jijini Nairobi wanaume ambao huona kivumbi kutoka kwa wake zao ni laki tatu. Lakini baadhi ya akina mama kutoka mkoa huo wanasema akina baba ndio wa kulaumiwa kwa kushindwa na majukumu yao ya kifamila. Wanasema waume wangi wamekuwa waume suruali tu. Hata hivyo wengi wanasubiri kuona kama kweli mgomo huo utafaulu, na ni wanaume wangapi walio na pesa za kwenda kula hotelini badala ya kula majumbani mwao.

Hali hii ni tofauti na hali ilivyo nchini Tanzania, kwani nchini Tanzania ni wanawake ndio wanaopigwa na kunyanyaswa mara kwa mara. Sijui itakuwaje wanawake wakiamua kugoma.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

chanzo. Waume waandaa mgomo

HAYA TENA WANAWAKE WA KI TANZANIA AMKENI NA NYINYI KUPIGA WAUME ZENU :lol::lol::lol:😛oa
 
mi kwakweli sielewi hawa wakinamama wananguvu kiasi gani cha kumcharaza mwanaume mpaka afikie hatua ya kugoma kula, kama hii ni kweli basi wanaume tumekwisha, tumebaki suruali tu...
 
Hata lucy ninawasi wasi huwa anamcharaza babu...lol...
 
huyo mwenyekiti naukubwa wote huo anatandikwa? kweli wanawake mtaua watu loh
 
Kumbe hata kwenye ndoa kuna ngumi :biggrin:
 
Back
Top Bottom