Kuna elimu fulani huwa najaribu kuwapa Watanzania lakini mlivyoganda kwenye ubongo huwa haiwaingii, mfahamu sisi tuna mitazamo ya kibepari, kwa kifupi sisi ni wafanya biashara, hatuna muda wa majungu au hata undugu. Mabepari huepuka uadui, hutumia namna yote kudumisha diplomasia ili wapige hela.
Nyie hapo mliharibiwa na ujamaa wa Nyerere, mnaishi kimajungu majungu hata baina yenu, kila kitu mnaendesha kwa visasi, sisi tuliposema kila anayeingia kwetu lazima apimwe, ikawauma mkaanza kulialia huku mkibwatuka na kung'aka, na kuanza kutafuta namna ya kulipiza kisasi, mlidhani hatua zetu tunazichukua kwa nia ovu kama mlivyo, mkasahau haja yetu kubwa ni kuhakikisha usalama wa kiafya kwa watu wetu.
Wakuu wa mikoa kwenu wakawa kila siku ni matamko ya vilio, ooohh mara tunawahujumu msipate watalii mara hiki mara kile, pumba tu. Sasa sisi kama mabepari au wafanya biashara huwa tunataka kila kitu kiende shwari bila makelele, hivyo ikabidi mkunwe kunwe na kutekenywa muache hayo makelele, rais wetu (mkali wa diplomasi) akampigia simu rais wenu, akamtekenya kisha mkaacha makelele, hali ikatulia, viongozi wakakutana, mkatekenywa zaidi na kucheka cheka kisha hali ikarudi kama kawaida.....nenda pale mpakani uone kinachotendeka, hakuna anayeingia kwetu bila wataalam wetu kumpima na kumhakiki.