Kasomi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 11,030
- 20,391
Kampuni binafsi ya uagizaji chanjo ya Sputnik V nchini Kenya inafikiria kuzirudisha Urusi chanjo walizoagiza.
Hatua hii inakuja wiki moja baada ya wizara ya afya nchini humo kupiga marufuku uingizaji au usambazaji na ugawaji wa chanjo dhidi ya corona kutoka vituo binafsi.
Dominic Kariuki, naibu mkurugenzi wa mamlaka ya dawa amesema kampuni imewaandikia ili kuona uwezekano wa kuzirudisha chanjo hizo.
“Kampuni iko kwenye mchakato rasmi wa kuomba kurejesha.Barua tayari imeletumwa kwa bodi ya maduka ya dawa na sumu,” Bwana Kariuki ameliambia baraza la seneti.
Katibu kuu wa Afya, Rashid Aman alisema amepokea dozi ya kwanza ya chanjo na watapokea dozi ya pili baada ya wiki tatu.
“Hii itawahusu watu 527 pekee ambao walichanjwa kabla ya marufuku ya chanjo hizo kutangazwa,” Bwana Aman alisema.
Shirika la Afya Duniani limependekeza kuwa chanjo zisichanganywe.