Kenya Yafungua Tawi La Bandari Kigali Rwanda

Kenya Yafungua Tawi La Bandari Kigali Rwanda

kusema kweli, nilisikia taarifa ile jana, wanasema wanataka kutageti usafirishaji kupitia bandari ya Mombasa kwa mizigo ya uganda,Rwanda, burundi na DRC. Tz wametuachia Zambia peke yake, malawi nayo mara nyingi inapitishia mizigo yake mozambique na south africa. utakuja kuona kuwa, hata vizuizi vingi ambavyo kenya wameondoa barabarani, hapa tz tunavyo vingi mno hadi unapokuwa unasafiri unapoteza muda mwingi. ukianza kusafiri mfano toka hapa dsm kwenda mwanza, kwenye weigh bridge utakuta mafoleni, kuanizia tu hapo kibaha, nenda chalinze, nenda moro, nenda dodoma, singida, Tinde shindayanga na ile ya mwisho kuingilia mwanza....balaa tupu, muda mwingi unapotea. kama issue ni kuwa makini katika ugaguzi na kudhibiti ukwepaji wa kodi au uzidishaji uzito wa mizigo, wangetafuta njia nyingine ya kisasa mbadala ambayo nchi zingine duniani wanazitumia na kuwa successiful bila kupoteza muda kiasi kile. Mwakyembe please, tusaidiane kupambana na hao jamaa katika competition. nafikiri wameamsa zaidi baada ya kusikia fununu kuwa bagamoyo itajengwa bandari itakayowafunika kabisa wale mombasa. Mungu ibariki Tanzania.

mbona hayo malori hayasimami ktk kila kizuizi!? kwa mwendo mrefu hadi kanda ya ziwa, yanasimama kwenye vizuizi viwili tu. kwengine wanaonesha ushahidi wa fomu na muhuri waliogongewa kwenye vizuizi vilivyo tangulia. banadari ya dar inaweza kushughulikia kontena 20 kwa saa, Mombasa 48 lkn ya bgmoyo itashughulikia zaidi ya 500 kwa saa. tuna mtandao mzuri wa barabara hadi kongo. Rwanda na Burundi kuliko Kenya. barabara za Kenya ni mbovu sana. Kenya wanajua kuwa ktk miaka 4 ijayo, Tanzania itatisha sana kimaendeleo ktk ukanda wetu huu. Malawi na Zambia bado zitaendelea kutumia bandari zetu. bandari ya mtwara inaboreshwa na ina kina kirefu. ushahidi ni meli kubwa ya maomba ya gesi iliotia nanga hivi majuzi. hata hivyo uhamasishaji wetu uendelee kuwavutia majirani kutumia bandari zetu
 
sidhan kama DRC na burundi wanaweza pitisha mizigo yao kupitia mombasa!!!! ila its a good move ktk kuondoa ubabaushaj kwa kua na office huko!!!
 
Hebu subiri kidogo labda sijakuelewa.Yaani unasema mizigo yote ya DRC na Burundi iwe inapita Rwanda????

Ya maana yake ni mizigo hiyo itapakuliwa mombasa kisha itasafirishwa mpaka Kigali ikipitia Uganda kisha itasambazwa DRC NA BURUNDI Ndio maana ya hcho kituo kujengwa Kigali.
 
tz iendelee na siasa za kodi kwenye line za simu , majirani wanaendeleza uchumi wao.
 
Ya maana yake ni mizigo hiyo itapakuliwa mombasa kisha itasafirishwa mpaka Kigali ikipitia Uganda kisha itasambazwa DRC NA BURUNDI Ndio maana ya hcho kituo kujengwa Kigali.

Na DRC na Burundi wameridhia kitu hicho? Mizigo yenyewe imekuwa specified au ni yote tu including silaha za kivita?Mbona sasa watakuwa wanampa hela awashikie mdeni wao?
 
Nyie watanzania wenzangu mnapenda sana siasa ndio maana hatuendelei. Huoni hata hii mada ni ya forum ya Business lakini mnaileta hapa kwa kina Ben Saanane hehehe.

Kwani hujui siasa ndo baba wa mambo yote?....Siasa ndo zimeharibu bandari ya Dar-es-salaam.Maamuzi ya kufungua tawi la bandari ya Mombasa Kigali yamefanywa na wanasiasa pia.Hata huu usingizi wetu wa pono ni wakisiasa tu!
 
View attachment 103724

BANDARI YA MOMBASA KENYA WAMEFUNGUA OFFICE KIGALI-MWAYKEMBE SISI TUMEJIPANGAJE?
Moja ya sababu inayotufanya tuendelee kuwa maskini ni hili la akili yetu kuiegemeza kwa wanasiasa....na ajabu ya mwaka unaweza kuta hata decision makers wa TPA nao wanatoa comment kama zako za kumhoji Mwakyembe!!

Bandari ni Mamlaka kamili yenye wataalamu na watendaji wa aina mbalimbali na wala sio Mwakyembe! Hawa ndio wanaotakiwa kuwa creative na kupeleka Propasal serikalini....hapo ndipo inapofuata role ya akina Mwakyembe! Pale bandarini kuna watu waliosoma Ports Management, Transport Management, Investment, Planning na mambo mengine kedekede! Pale kuna Directorate of Planning and Investment; hawa ndio wanaotakiwa ku-explore different opportunities available kisha kupeleka proposal zao kwa akina Mwakyeme! Tusizani safari zote za akina Obama kuja Afrika zinakuwa initiated serikalini, la hasha....zingine zinakuwa initiated na government institutions na hata wafanyabiashara!! Kwa hapa Tanzania, taasisi za serikali kama TPA ndio wanaotakiwa ku-explore hizi opportunities na kisha kupeleka proposal serikalini.....huko zikataliwe ndipo tuje kuwahoji akina Mwakyembe! Siamini mtu kama Mwakyembe anaweza kuikataa productive project....
 
mbona hayo malori hayasimami ktk kila kizuizi!? kwa mwendo mrefu hadi kanda ya ziwa, yanasimama kwenye vizuizi viwili tu. kwengine wanaonesha ushahidi wa fomu na muhuri waliogongewa kwenye vizuizi vilivyo tangulia. banadari ya dar inaweza kushughulikia kontena 20 kwa saa, Mombasa 48 lkn ya bgmoyo itashughulikia zaidi ya 500 kwa saa. tuna mtandao mzuri wa barabara hadi kongo. Rwanda na Burundi kuliko Kenya. barabara za Kenya ni mbovu sana. Kenya wanajua kuwa ktk miaka 4 ijayo, Tanzania itatisha sana kimaendeleo ktk ukanda wetu huu. Malawi na Zambia bado zitaendelea kutumia bandari zetu. bandari ya mtwara inaboreshwa na ina kina kirefu. ushahidi ni meli kubwa ya maomba ya gesi iliotia nanga hivi majuzi. hata hivyo uhamasishaji wetu uendelee kuwavutia majirani kutumia bandari zetu
Watzoo ni mitu ya maneno mingi eti bandari ya Bagamoyo itahudumia kontena 500 ipo? eti barabara zetu ni nzuri kuliko za Kenya na Rwanda, ulishafika Kenya au tukuwekee projects za barabara za Kenya na viwanja vya ndege vinavyojengwa sio bandari zetu za kwenye makabrasha, ni ujinga huu huu unaotufanya tupumbazike bila kuongeza bidii tufanane na wenzetu.
 
Daaah...hii habari imeniumiza sana roho kwa kweli....hawa jamaa wana mipango haswa na sisi tumelala sana....waliposikia tu tunataka kutoa kitu kipya pale Bagamoyo wamekuja na hii strategy mpya.What is our next move?
 
Tanzania wrapped up in itself makes an upleasant bundle! Ili ule kubali uliwe quote JK.
 
Daaah...hii habari imeniumiza sana roho kwa kweli....hawa jamaa wana mipango haswa na sisi tumelala sana....waliposikia tu tunataka kutoa kitu kipya pale Bagamoyo wamekuja na hii strategy mpya.What is our next move?

Hapo our queen is under check inabidi tucheze kete ya akili sana hapo.
 
aliyelala usimwamshe, acha tuendelee kulala
 
Daaah...hii habari imeniumiza sana roho kwa kweli....hawa jamaa wana mipango haswa na sisi tumelala sana....waliposikia tu tunataka kutoa kitu kipya pale Bagamoyo wamekuja na hii strategy mpya.What is our next move?

Checkmate Bandit! Checkmate Bandit!
 
Watzoo ni mitu ya maneno mingi eti bandari ya Bagamoyo itahudumia kontena 500 ipo? eti barabara zetu ni nzuri kuliko za Kenya na Rwanda, ulishafika Kenya au tukuwekee projects za barabara za Kenya na viwanja vya ndege vinavyojengwa sio bandari zetu za kwenye makabrasha, ni ujinga huu huu unaotufanya tupumbazike bila kuongeza bidii tufanane na wenzetu.

inaelekea hujuii unacho kisema. malori huwa yanatumia barabara ya Mombasa, voi, Nairobi, nakuru, kericho, Kisumu hadi busia. hii barabara nimeitumia sana na wiki 2 zilizopita nilisafiri toka Nairobi hadi mbale, Uganda. mashimo ni mengi sana. acha kudanganya watu. tunazungumzia barabara siyo majengo. tunazungumzia barabara siyo viwanja vya ndege. hizo kontena zitabebwa na ndege. licha ya kuwa nchi kubwa kuliko zote, Tanzania ina mtandao wa barabara nzuri kuliko Kenya na uganda
 
Hapo our queen is under check inabidi tucheze kete ya akili sana hapo.
Wenzetu wanaendesha public sector zao with a private sector mentality...ndo maana KQ(Kenya Airways)kuifananisha na Air Tanzania ni kufananisha kifo na usingizi.Sisi hatupo hivyo..by then TTCL ilikuwa na wafanyakazi wengi kuliko hata celtel Africa(bila kujali ufanisi na kubana matumizi nk),matokeo yake TTCL ilishindwa ku-deal na private mobile operators.I can see the same coming to haunt TPA na nchi kukosa mapato na watu kukosa kazi
 
mbona hayo malori hayasimami ktk kila kizuizi!? kwa mwendo mrefu hadi kanda ya ziwa, yanasimama kwenye vizuizi viwili tu. kwengine wanaonesha ushahidi wa fomu na muhuri waliogongewa kwenye vizuizi vilivyo tangulia. banadari ya dar inaweza kushughulikia kontena 20 kwa saa, Mombasa 48 lkn ya bgmoyo itashughulikia zaidi ya 500 kwa saa. tuna mtandao mzuri wa barabara hadi kongo. Rwanda na Burundi kuliko Kenya. barabara za Kenya ni mbovu sana. Kenya wanajua kuwa ktk miaka 4 ijayo, Tanzania itatisha sana kimaendeleo ktk ukanda wetu huu. Malawi na Zambia bado zitaendelea kutumia bandari zetu. bandari ya mtwara inaboreshwa na ina kina kirefu. ushahidi ni meli kubwa ya maomba ya gesi iliotia nanga hivi majuzi. hata hivyo uhamasishaji wetu uendelee kuwavutia majirani kutumia bandari zetu

Kama bandari ya Bagamoyo itakuwa na uwezo wa kuhudumia konteina 500 kwa saa, kwa muda wa saa 12 watahudumia kontainer 6000 ambazo ni sawa na tani 120,000 (assuming 20ton weight for one container).

Tutakuwa na uwezo wa kusafirisha tani 120,000 kwa siku ukichukulia kwamba sasa kwa reli hivi tunasafirisha tani pungufu ya 500,000?!
 
Back
Top Bottom