scramble
JF-Expert Member
- Nov 29, 2012
- 1,593
- 257
kusema kweli, nilisikia taarifa ile jana, wanasema wanataka kutageti usafirishaji kupitia bandari ya Mombasa kwa mizigo ya uganda,Rwanda, burundi na DRC. Tz wametuachia Zambia peke yake, malawi nayo mara nyingi inapitishia mizigo yake mozambique na south africa. utakuja kuona kuwa, hata vizuizi vingi ambavyo kenya wameondoa barabarani, hapa tz tunavyo vingi mno hadi unapokuwa unasafiri unapoteza muda mwingi. ukianza kusafiri mfano toka hapa dsm kwenda mwanza, kwenye weigh bridge utakuta mafoleni, kuanizia tu hapo kibaha, nenda chalinze, nenda moro, nenda dodoma, singida, Tinde shindayanga na ile ya mwisho kuingilia mwanza....balaa tupu, muda mwingi unapotea. kama issue ni kuwa makini katika ugaguzi na kudhibiti ukwepaji wa kodi au uzidishaji uzito wa mizigo, wangetafuta njia nyingine ya kisasa mbadala ambayo nchi zingine duniani wanazitumia na kuwa successiful bila kupoteza muda kiasi kile. Mwakyembe please, tusaidiane kupambana na hao jamaa katika competition. nafikiri wameamsa zaidi baada ya kusikia fununu kuwa bagamoyo itajengwa bandari itakayowafunika kabisa wale mombasa. Mungu ibariki Tanzania.
mbona hayo malori hayasimami ktk kila kizuizi!? kwa mwendo mrefu hadi kanda ya ziwa, yanasimama kwenye vizuizi viwili tu. kwengine wanaonesha ushahidi wa fomu na muhuri waliogongewa kwenye vizuizi vilivyo tangulia. banadari ya dar inaweza kushughulikia kontena 20 kwa saa, Mombasa 48 lkn ya bgmoyo itashughulikia zaidi ya 500 kwa saa. tuna mtandao mzuri wa barabara hadi kongo. Rwanda na Burundi kuliko Kenya. barabara za Kenya ni mbovu sana. Kenya wanajua kuwa ktk miaka 4 ijayo, Tanzania itatisha sana kimaendeleo ktk ukanda wetu huu. Malawi na Zambia bado zitaendelea kutumia bandari zetu. bandari ya mtwara inaboreshwa na ina kina kirefu. ushahidi ni meli kubwa ya maomba ya gesi iliotia nanga hivi majuzi. hata hivyo uhamasishaji wetu uendelee kuwavutia majirani kutumia bandari zetu