Kenya yageukia Falme za Kiarabu kwa ajili ya kupata fedha za kukamilisha ujenzi wa reli ya kisasa

Strong ladg

Senior Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
170
Reaction score
445
Kenya imeanza mazungumzo na Umoja wa falme za kiarabu ( UAE) kwa ajili ya kupata fedha za kukamilisha ujenzi wa reli ya kisasa ( SGR).

Kenya imeamua kuigeukia UAE baada ya China iliyokuwa ikitoa fedha kwa ajili ya mradi huo kuamua kujitoa.
Ujenzi wa reli ya kisasa inayokusudiwa kuunganisha bandari ya Mombasa na nchi jirani zisizokuwa na bandari ulikwama mwaka 2019 kutokana na ukosefu wa fedha.

Vilevile UAE inakamilisha taratibu za kuipatia Kenya mkopo wa Dola za Marekani Bilioni 1.5 Ili kusaidia masuala ya kibajeti.

Wiki hii Rais William Ruto alikuwa ziarani katika falme za kiarabu ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa UAE pamoja na kusaini mkataba wa ushirikiano wa kibiashara kati ya Kenya na Umoja wa falme za kiarabu

Source: - https://www.monitor.co.ug/uganda/ne...ilway-funds-after-china-cut-financing-4890188
 
No baada ya Uganda kuwaambia wakatafute hela Kwa Mwarabu ambae ndio anawafadhili na wao.
 
Anko Magu kwetu alicheza kama pele…Hongera zake mwamba huko aliko🙌🙌
 
Ujenzi wa Viwanja AFCON 2027 wanakuja kukopa Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…