Kenya Yaibuka Nafasi ya Pili Dunia Katika Mashindano ya U20 Oregon

Kenya Yaibuka Nafasi ya Pili Dunia Katika Mashindano ya U20 Oregon

OwadeKuya

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
535
Reaction score
312
Mashindano ya Dunia ya Riadha kwa wanariadha walio chini ya miaka 20 yaliyofanyika Eugene, Oregon, Marekani, ikimaliza nafasi ya pili kwenye jedwali la medali.
Timu Kenya ilijikusanyia medali 11—dhahabu 4, fedha 3 na shaba 4—ikifuatiwa na wenyeji Marekani waliotwaa medali 24. Kenya pia ilikuwa taifa la Afrika lililofanya vizuri zaidi, huku Ethiopia ikimaliza nafasi ya tano ikiwa na medali 6.

Walioibuka washindi wa dhahabu:
Frankline Kibet – 5,000m wanaume
Emmanuel Kiprono – 3,000m wanaume
Wilson Chepkwech – 1,500m wanaume
Josephine Sembeyo – 1,500m wanawake
Medali za fedha zilinyakuliwa na David Kapaiko, Nehemiah Kipng’eno na Emmanuel Lemiso.
Medali za shaba zilipatikana kupitia Nicholas Kitum, Caren Chepchirchir, Joyline Chepkemoi na Anatasha Cheptoo.

Mwenyekiti wa Athletics Kenya anayesimamia maendeleo ya vijana, Barnaba Korir, amepongeza wanariadha, makocha, familia na timu nzima kwa kupeperusha bendera ya Kenya kwa fahari.
Korir amesema matokeo hayo yanaonyesha kuwa Kenya ina hazina kubwa ya vipaji vya vijana na kutoa matumaini ya mustakabali mzuri wa riadha nchini.
Hongera Team Kenya!
Source : The star
 
Back
Top Bottom