Nuel27
JF-Expert Member
- Jul 3, 2026
- 461
- 915
Kenya imesaini makubaliano ya kuagiza tani 540,000 za mahindi kutoka Zambia ili kuongeza upatikanaji wa nafaka hiyo baada ya uzalishaji wa mahindi meupe nchini Kenya kushuka hadi kiwango cha chini zaidi katika kipindi cha miaka saba. Kwa zingatio la makubaliano hayo, Zambia itauza mahindi ya Daraja A yasiyobadilishwa vinasaba.
Mahindi hayo yatasafirishwa kwa awamu sita: shehena tano za tani 100,000 kila baada ya miezi mitatu, na shehena ya mwisho ya tani 40,000. Makubaliano hayo yamekuja wakati Kenya ikizingatia kuruhusu uagizaji wa hadi tani milioni 3 za mahindi bila ushuru wa forodha ili kukabiliana na upungufu wa mahindi nchini humo. Taarifa hiyo ni kwa Waziri wa Kilimo wa Kenya, Mutahi Kagwe.
Makubaliano kati ya Zambia na Kenya yanatarajiwa kuimarisha biashara ya nafaka katika kanda chini ya mfumo wa Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA). Hatua hiyo itaipa Zambia soko jipya kubwa la mazao yake huku ikiisaidia Kenya kupata chakula muhimu kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya wananchi wake.
Kwa mantiki hiyo mahindi yatakuwa yanatoka Zambia kupita Tanzania nchi ambayo inalima mahindi kwa wingi nadhani kushinda hata Zambia then yataenda mpaka Kenya
Nadhani kuna mahala kuna kitu hakiko sawa ,wajuzi wa mambo naomba mtujuze kwa nini biashara isingekuwa kati ya Tanzania na Kenya 🙏