Ndugu quality strategic decision ni data and use of data to interpret finding ndioresearch. Iwe ni days za ndani ya kampuni, za soko au za serikali.
Ufundishwi research methodology kwa sababu ya kuandika dissertation tu; unatakiwa utumie hizo skills mbele kwenye ajira huko mbele au ukiwa kwenye strategic decision making position.
Maamuzi ya strategic yanahitaji data na hakuna mtu mwenye uwezo wa ku-compile data kama serikali, sasa kuitisha makongamano na kudhani hiyo ndio source kuu ya maamuzi ya kibiashara au dira ya uchumi ni ujinga to say the least.
Shida yako ni kudhania vitu kutoka kichwani kwako badala ya kufahamu how things work in the world.
SAHIHI
Unamwangaza sana...
Kujenga taasisi imara ni jambo linalofungamana na upeo na uwezo wa kutafsiri 'sura na mienendo' ya mambo kwa data fasaha; na tena(1) za msingi na (2) kwa uweledi katika kuzisaka, kuzitumia na kuzichambua...
Hili nalo ni suala lenye mengi ya ulazimu wa miundo thabiti ya kiutendaji, maamuzi na utekelezaji--ni kweli kuna tatizo la 'dhana ya ushirikishwaji' katika mambo nyeti ya 'kupanga maendeleo' hapa kwetu na khasa katika muktadha wa 'mashauriano ya watendaji na wanajamii' ,
consultations, yanapohusisha umma usio 'Elimu ya Kina Mambo'...
Uzoefu wa miye kama mtu kuwa katika shughuli za jamii na miradi, umenipatia utambuzi wa jinsi 'Ukosefu wa Elimu ama mapana ya uelewa' katika jamii ni gharama kiuchumi na fedha na fadhaa ya kiutamaduni; kuna namna, 'jamii isiyo na taamuli'--mambo ya kujifahamu, inaponza utendaji wote mzima wa serikali na jamii yenyewe.
'Jamii isiyo na taamuli' ni jambo mtambuka... Linaathiri shughuli za serikalini na za jamii; unapoona watu wanajihesabia 'usomi' na kumbe usomi wenyewe ni utundu tu wa maandiko na 'kusukuma siku' katika shughuli za maendeleo ni dalili ya 'Elimu ya Mchongo' kutamalaki katika suala zima la 'kuelimishana' na 'kupeana madaraja jina/uhitimu'--jambo la kupelekea aibu ya kukosa uweledi wa kweli na tena kukosa dhamira ya kujifunza ili kukwamua adha za kimaisha katika jamii imzungukayo mtu--ile kwa dhati...
Kwa hivyo, unapatia hasa unapokosoa mambo ya 'ukosefu wa uweledi' katika fani, utumishi na karia...
Ikiwa kuna la kushauri katika hili; ni kukazia umuhimu wa 'Taamuli katika Jamii'--mambo ya 'Mwenge wa Uhuru'...
Sasa mambo ya 'Taamuli katika Jamii' ni ujumuifu wa imani, elimu bora na roho ya kujizatiti katika utumishi/kazi/huduma na matendo...
Kiufundi, mambo mengi ya migogoro ya kijamii , iwe Tanzania ama kungineko, hayatatatuliwa, kwa 'elimu' na 'uongozi' kwa sura ya kileo ya mambo--hata kudai
utaasisi wa demokrasia ya kiliberali; kwa kuwa khasa, udhahiri wake ni mambo yanaweza kutatuliwa kupitia 'ukombozi wa kifikra' na 'imani'...
Umahiri katika kazi na huduma unakwamishwa na elementi ya makusudi yenye kuharibika katika mambo kama vile umendeaji mbovu wa nafasi za ajira, utumishi, uongozi, utendaji n.k miongoni mwa wanajamii wenyewe--mambo ya jamii na utamaduni.
Rushwa na mmomonyoko wa maadili ndiyo kiini cha kufubaza jitihada za dhamira za kimaendelo ya kweli.
Ni rahisi hata kubaini 'maandiko yenye usanii' katika utayarishaji wa 'Miradi ya Maendeleo' na tena 'utendaji wenye usanii' kufuatia 'utekelezaji wake'... Lakini nani amfunge paka kengele?
... Katika ulimwengu wa leo wa 'Uchumi Mauti' kila kitu ni 'Usanii' na kulana danzu...
'Mikakati' ni jambo linalotaka umakini katika Mipango na miongozo ya Utendaji, sera na sheria makini, na basi kudhibiti mianya ya 'usanii' katika utekelezaji; hili ni kwa maslahi mapana ya jamii nzima 'yenye kujielewa' vema ama sivyo ni mwendo wa muktadha akilifu wa kompromaizi kati ya 'watawala' na 'wataliwa'. Hivyo basi maslahi ni ugani wa mambo ya nyakati, utendaji na makusudi -- kwa sura pana, ya muda mfupi na pia muda mrefu... Wakati huo huo mikakati ni sanaa ya 'mapiku' kwa wale 'wanaojifahamu ilivyobora'--jambo linalohitaji 'kukesha macho'...