Analogia Malenga
Platinum Member
- Feb 24, 2012
- 5,292
- 10,842
Serikali ya Kenya imetoa wito kwa serikali ya Uganda kufanya uchunguzi huru kwa raia wawili wa Kenya waliotekwa na kupitea nchini Uganda ambao hadi sasa hawajulikani walipo. Bob Njagi na Nicholaus Oyoo walikamatwa katika Kituo cha Mafuta na watu waliokuwa na silaha ambapo baada ya kutekwa simu zao zilizimwa hadi hivi leo hawajapatikana tena.
Madai ya Kenya ni kuwa kesi iliyofunguliwa mahakama kuu ya Uganda ilitupiliwa mbali kwa kilichodaiwa kukosekana kwa ushahidi. Hivyo Kenya imetoa wito kwa Uganda kufanya uchunguzi huru kwa raia hao. Kenya imesema ina wajibu wa kulinda raia walioko ndani ya mipaka ya Kenya na nje ya mipaka.