Kenya yaongoza Afrika Mashariki kwa kuwa na furaha. Congo DR na Tanzania hazina furaha kabisa.

Kenya yaongoza Afrika Mashariki kwa kuwa na furaha. Congo DR na Tanzania hazina furaha kabisa.

Furaha inatoka wapi na wakati kuna utopolo kibao unaendelea, mara utekaji, CCM na Chadema hawa hapa, mara Karia na genge lake, illiterates kibao ukimwelesha jambo haelewi.

Acha tu mkuu tutafika
 
...
 

Attachments

  • IMG-20250322-WA0014.jpg
    IMG-20250322-WA0014.jpg
    105.3 KB · Views: 31
Furaha itoke wapi kwenye nchi ambayo haki Yako unapewa kana kwamba umehurumiwa
Kila mtu kwenye sehemu yake anafurahia kumnyanyasa muhitaji useme furaha iwepo!?
Ukinunua ka uwanja mahali unakuwa huna uhakika kama kweli ni halali au sio halali wizi na utapeli umetamaraki
 
SA wana furaha miji mingine saa moja watu wapo ndani kama kuku na kutoka kuanzia saa mbili muda ambao shift mpya ya police inakua washaanza kazi ukiwa road saa moja asubuhi utakutana na wazee wa kazi.
 
Nchi iongozwe na mifumo ya kishetani, halafu watu wawe na furaha? Haiwezekani. Shetani huwaletea furaha mawakala wake kama hawa machawa eanafiki, wauaji na watekaji, wapokeaji wa rushwa za mauzo ya bandari, mbuga za wanyama na hifadhi za misitu yetu.

Kwa watu waungwana na wazalendo kabisa, na wenye Roho wa Mungu, Tanzania nzima, ni kipindi cha majuto na laana.

Kuondoka kwenye hali hii, ni NO REFORM.NO ELECTION.
 
Furaha inayozungumziwa hapa inajumlisha mambo mengi ikiwemo uchumi; kiwango cha rushwa; umri wa kuishi; huduma za afya n.k. kwa nchi husika. Watu ambao nchi zao zina uchumi mzuri wana nafasi kubwa ya kuwa na furaha kuliko wale walio katika hali mbaya kiuchumi. Nchi nyingi za Afrika zinaangukia katika kundi hili. Hivyo ukiitazama ramani ilivyo, utagundua kwamba nyingi za nchi ambazo watu wake hawana furaha kwa vigezo ambavyo watafiti wa suala hili wamevitumia wanatoka katika Bara hili. Afrika.
Lakini vigezo vilivyotumika vina kasoro zake pia.. Je, inakuwaje Israel inapata moja ya nafasi za juu katika jedwali hili? Kuna kigezo kimoja ambacho kinaangalia uhuru wa mtu kuamua maisha anayotaka ( freedom to make your own life choices). Uhuru huu ni pamoja na ushoga. Israel ni nchi ambayo suala hili limetamalaki sana na matamasha mkubwa ya mashoga wa ulimwenguni hufanyika huko. Kwa kigezo hiki pia Nchi za Afrika zinawekwa chini kwa vile hazikubaliani na uhuru wa aina hii.

Angalia pia nafasi ya USA katika jedwali hili. Wameporomoka kutoka nafasi ya 15 mwaka 2023 hadi ya 23 mwaka 2024. Mwaka 2025 watazidi kuporomoka kwani Rais wao hana mizaha katika suala hili.
Je, mwana JF bado unaamini kuwa sisi hatuna furaha kweli?
 
Back
Top Bottom