Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Kenya jana imetangaza kupunguza ada za kuingia mbuga kuu za wanyama pori kwa watalii kutoka ndani na nje ya nchi hiyo ili kuhimiza sekta ya utalii iliyoathiriwa sana na janga la COVID-19.
Taarifa iliyotolewa na Shirika la huduma za Wanyamapori nchini Kenya (KWS) limesema hatua hiyo itadumu kwa mwaka mmoja.
Pia shirika hilo limewaruhusu wamiliki wa nyumba za kulala wageni kwenye hifadhi za wanyama pori wasitishe kulipa kodi kwa mwaka mmoja kuanzia tarehe Mosi mwezi Julai hadi tarehe 30 mwezi Juni mwaka ujao.
Waziri wa utalii na wanyama pori wa Kenya Najib Balala amewataka wamiliki hao kuboresha huduma za watalii na kukuza biashara zao kwa kutumia akiba inayotokana na usitishaji wa kodi.