Kenya yatangaza kutopokea mahindi Tanzania na Uganda

Kenya yatangaza kutopokea mahindi Tanzania na Uganda

Soon ndege za Kenya zinapigwa ban hahaha
Rais wetu njoo huku umechokozwa...

........updates......
Maziwa ya unga yoka Kenya tayari yanajadiliwa kutoingizwa nchini
Hilo lazima litapita nilisikia juzi wakijadili kuwa tunayo na wataanza na taasisi za umma
 
You people, you are lucky i am not in Magufuli's position.

If it ever happened that i were the President Of this dear country of mine at this moment, then i would
Make Sure i bleed you white of your pomposity, obstinacy and propaganda against my country and Tanzanians
No matter how angry a chicken is, it'll never kill an eagle.
 
Mamlaka ya Kilimo na Chakula ya Kenya imesema uchunguzi umebaini kuwa mahindi yayoingia kutoka Tanzania na Uganda sio salama kwa matumizi ya wakenya

Wamesema mahindi hayo yana kiwango kikubwa cha mycotoxins, hasa aflatoxins na fumonisins ambazo yanajulikana kusababisha saratani

Sumu hizo zimesababisha vifo vya wakenya wengi kwa miaka, hali iliyosababisha wachukue hatua ya kuacha kupokea mahindi kutoka Tanzania na Uganda

Aidha wamesema wataendelea kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na nchi wazoshirikiana nazo kibiashara na wanasubiri kuona washikadau wakilizungumzia tatizo hilo
==
View attachment 1718222
Kwa hatua hii mpaka Wakenya wenzao wanawashangaa
20210307_161559.jpg
 
No matter how angry a chicken is, it'll never kill an eagle.

Soon we shall know who is reffered to as a chicken.

I asure u, in less than 2 days, the chicken is going to bow down and peck the spilled maize grains.
 
Sioni tatizo lolote hapo. Kwanza kwa nini Tanzania wanauza mahindi badala ya unga? Tutaongeza ajira kwa kuuza unga sio mahindi. Serikali irudi kwenye drawing board na kuanza kusitisha uuzaji wa mahindi nje ya mipaka ya Tanzania. Uwekwe mkakati hivi sasa kuwa na viwanda zaidi ili tuweze kuuza unga wa mahindi.
 
Tunapanda mahindi wenyewe na pakiwa na upungufu tunaweza kuagiza kutoka Mexico. Nyinyi hatuwahitaji sana.
Kenya haina uwezo wa kujitosheleza katika mshindi, labda waingie kutoka sehemu nyingine na kwa mwaka huu ni Tanzania pekee katika Southern Africa food pool ndio wenye ziada ya tani 3 million.

Uongozi hautakiwi uwe na haraka, wenye mshindi kwenye magari yanayo safirishwa mahindi ni wakenya .

Kenya watarudi tuu.
 
Tunapanda mahindi wenyewe na pakiwa na upungufu tunaweza kuagiza kutoka Mexico. Nyinyi hatuwahitaji sana.
Hiyo kwenu itabaki kua short term plan, the only solution ni kujilisha kwa 100% otherwise nyi mtabaki kua customers wa tz
 
Nimeshindwa kuelewa kipi kimeharibu soko la mpunga maana mahindi inajulikana Zambia ila mpunga Hadi sasa sijui kuna shida gani
mkuu tokea Covid ianze tumesuswa sijui kwanini......


kuna wakati nahisi kauli za mzee 'wao wamejifungia sisi tulime mazao wakija kununua tunawatandika bei' zitakua ziliwakera walio wengi!


huyu baba ameua kabisa uti wa mgongo wa nchi hii, diplomasia inakoenda sielewi
 
Inauma, maana watu wetu wanakufa kwa saratani halafu mijinga inapokea hela ili ihakikishe ubora wa kile tunanunua kutokea kwenu huko, na kwa mlivyo wazembe mnasindika magunia tu, wala hamkai mfikirie au kutumia ubongo.
Sawa! Sasa Tanzania ipige marufuku mazao yote ya kuliko kupelekwa kenya.
 
Sawa! Sasa Tanzania ipige marufuku mazao yote ya kuliko kupelekwa kenya.

Halafu Waganda wamepiga kimya na kutafuta namna za kitaalam kukabili hii issue na kubaini ukweli, Watanzania ndio wamepiga ukunga, siku zote ukishutumiwa kwa chochote, kabla kulipuka kwa maneno mengi, shona mdomo kwanza sklizia na kujua upepo unavuma kwenda wapi.
 
Tunapanda mahindi wenyewe na pakiwa na upungufu tunaweza kuagiza kutoka Mexico. Nyinyi hatuwahitaji sana.
Huyo umemjibu sahihi kabisa, nadhani ni mmoja kati ya wajinga tulionao hapa kwetu.

Lakini kuna swala la msingi zaidi kuliko huo ujinga alioandika hapo, na kwa bahati mbaya hata wewe naona unaungana naye kwenye ujinga wake kwa jibu ulilompa.
Je, kuagiza Mexico ndio suluhisho kwenu?

Nadhani ungeanzia kwenye hao maofisa wenu waliochukua uamzi huo. Naona barua yenyewe haielezi lolote la msingi katika utekelezaji wa jambo kama hili katika ushirikiano tulio nao.

Je, hawa maafisa wenu wamejiridhisha kwamba wamefuata taratibu zote zilizopo katika kutekeleza upigaji marufuku huo?

Kinachoonekana hapa ni kama maofisa wenu ni uzalendo (?) ndio umewalemea zaidi ya kitu kingine chochote. Wanalinda maslahi ya wakulima wa Kenya zaidi, hata kinyume cha taratibu zilizokubarika kwenye ushirikiano wa nchi hizi za EAC.

Hapa mmepotea sana. Hakuna cha kujivunia hapa.

Sawa, nendeni mkanunue mahindi Mexico, but at what price? (sina maana ya bei ya juu kwa gunia moja la mahindi).
 
Halafu Waganda wamepiga kimya na kutafuta namna za kitaalam kukabili hii issue na kubaini ukweli, Watanzania ndio wamepiga ukunga, siku zote ukishutumiwa kwa chochote, kabla kulipuka kwa maneno mengi, shona mdomo kwanza sklizia na kujua upepo unavuma kwenda wapi.
Waganda siku zote mmezoea sana kuwaonea.

Usidhani mnao ubavu wa kuwaonea waTanzania kama mnavyowafanyizia waganda.

Hivi kwa nini hamtaki kujifunza na kuelewa hivyo?

Nakushangaa hadi hapa bado hujaona jinsi maofisa wenu walivyokosea stepu.
 
Hapa ndo huwa nampendea Magufuli aisee, huwa haniangushi kabisa, maake mzee hapigagi magoti kabisa, nafikiri tutegemee warudi wakiomba msamaha maake hawaachagi kujitoa ufaham kisha wanarejea tena wakisugua magoti na majuto yasiyo kifani, tuongoje wakati tu uzungumze.
Kwenye hili ningependa wapewe somo ambalo hawatalisahau milele.

Tena wamekosea 'timing' vibaya zaidi.

Wao ndio wenyekiti wa EAC, halafu mtu wao ndio kaingia kuwa Secretary General. Mbona kazi yao wanaifanya iwe ngumu zaidi?
 
Madai yanaweza kuwa kweli. Lakini si wangeiambia serikali kuwa bidhaa hii ina mapungufu fulani yarekebishwe?
Hapa kale kamchezo hakajaisha. Wataacha ya Tz watatachukua Uganda kimyakimya. Lengo ni kuitosa Tanzania.

Sisi wakulima wa mahindi tumekwisha.
"Sisi wakulima wa mahindi tumekwisha."

Pole sana mkuu 'Lihakanga'; lakini inasikitisha kujiweka kitumwa kiasi hiki!

Kwa hiyo bila Kenya ukulima wa mahindi hapa kwetu hakuna? Ina maana Kenya akikohoa, kama alivyofanya hivi sasa, sisi tuwe na homa kali kabisa?

Badala ya kuwaonea huruma nyinyi wakulima, kwa fikra za namna hii badala yake zinaamsha hasira. Hatuwezi kuwa taifa la kujikweza namna hii.

Soko linapatikana Kenya peke yake? Mbona wao wanatafuta sehemu mbadala za kununua, kwa nini nasi tusitafute sehemu mbadala za kuuza?

Hatuwezi hata kuwalisha ngurue ili tushike soko la nyama ya nguruwe eneo la ukanda huu?

Hatuwezi kuwekeza kwenye kutengeneza 'ethyl alcohol' ya kuchanganya na petroli kuweka kwenye magari?

Lakini tunapenda sana kazi rahisi hii ya kufanya biashara huku ukisutwa utu wako, eti mradi unapata hela?

Hawa watu ni wapuuzi sana, na wataendelea kuwakalia vichwani na kuwatukana, hata vizazi vyenu vyote mtatukaniwa.

Achana na akili za kitumwa na kitwana za namna hiyo.
 
Back
Top Bottom