Wadau wabongo, hii thread imeanzishwa ili kuonyesha nani ana ubavu katika makazi mazuri, nina uhakika sisi wenyewe tunapost hapa ila kwetu hatukai nyumba za aina hizi na huwa tunaona tuu ukipita karibu, real estate nairobi ni business inayokomaa na ndio unaona haya makazi mazuri, hivyo basi hata hivyo haijaanza siku nyingi ndio maana maeneo yete tunayoona ni mapya na mengine yapo katika hatua za mwisho za ujenzi, naamini bongo kuna maeneo kama haya mengi ila sisi hapa bongo kila mtu huwa anajenga nyumba yake kwa kubangaiza , mfano mtu anaanza na kiwanja au anaanza na kununua tofali moja moja na anadunduliza mpaka ananyanyua chumba kimoja kwanza, kama umeangalia habari hivi juzi juzi, kuna mabenki kama nane yamesign mikataba kuanza kutoa mikopo kwa ajili ya kununua nyumba hivyo basi kwa muda mfupi unaokuja tegemea housing boom tanzania, mambo yanayofanyika nairobi na kenya kwa ujumla yanakuja na dar muda si mrefu ila tu wenzetu wametangulia kidogo, hii isitufanye tunaanza kujidharau wenyewe, angalia maofisi sasa hivi jijini dar kila eneo yanchipuka, na makazi bora pia yanakuja, kuna nyumba zaidi ya 300 kule maeneo ya kijichi au karibu na mbagala ni za nssf kama kuna mtu atapiga picha hakuna tofauti na zile za nairobi, pia kigamboni kuna miradi mingi, ila tu wabongo hata hawapost picha wanashangilia tuu, yaani utafikiri mechi inachezewa kwao na wanashangilia timu ngeni, upanga sasa hivi kuna magorofa kibao ni residential zile, watu wakipost wabongo wanalalamika, pia kariakoo, ngoja niishie hapa kwanza.