Kenyan & Tanzanian Surburbs

Kenyan & Tanzanian Surburbs

Coco Beach Dar es Salaam

Dar lagoon.jpg
dar beachtrees.jpg
dar beaches 2.jpg
Dar road.jpg
 
Kweli wakenya kwenye swala hili wametuzidi,inabidi tukubali tu,maana sisi tuna nyumba moja moja nzuri,si mtaa mzima,ndio maana swala la kuweka picha hapa yenye mitaa yetu inakuwa tatizo.
Huko tunakosifiaga oysterbay,masaki,sijui nyiro n.k hakuwezi wafikia hawa jamaa,wao wapo next level,kuanzia mpangilio wa mitaa,utunzaji wa maringira n.k.
Pili naona ndugu zangu watz wanakosea-kuna watu wamepost picha za maghorofa na majengo mengine ya biashara,naona wanakosea,wekeni picha za mitaa yenye makazi ya watu,si kupost picha za majengo kama za quality center
 
Tunaonesha mazuri tuliyonayo (mfano bichi) ambayo wenzetu wa Nairobi hawana
lakini nairobi ni part ya kenya-na kenya wana bahari,ndo maana ukicheki kwenye baadhi ya picha za zilizopostiwa humu kuna zinazoonyesha beach pia,cheki picha za mombasa
 
Dar es salaam sio sehemu ya kuilinganisha na NRB hata kidogo, ukienda hapo kariakoo majengo yapo yapo tu utadhani Afghanistan, vilevile barabara bara hazipitiki utadhani hatuna viongozi. Cha muhimu hapa ni kwamba uwezo tunao isipokuwa Miji yetu Tanzania tunaijenga bila mpangilio. Wenzetu Kenya wamethubutu , wakaweza na sasa wanasonga mbele, hiii yote ni kwa sababu ya kuwa na viongozi imara wanaoweza kufuata maadili ya kazi, pia elimu nayo imechangia mpaka wakafika hapo, kule kenya kila mtu anachakarika kutafuta ridhiki , wanaheshimu sana kazi inayowapatia mlo hata kama iwe ni kuzibua mavi, ukilinganisha mf: na wakazi wa Dar wapo wapo tu , wanaishi kiujanja ujanja na kutapeli hawataki kujishughulisha. kiufupi sisi ni wavivu wa kufanya kazi na hata kufikiria na ndio maana tuko kwenye hali duni kama hii.

Bila kusahau kitu kingine kinachofanya wenzetu wawe mbele namna hiyo ni pamoja na kuwa na soko kubwa la utalii duniani, leo hii ukitembelea hata ulaya mpaka vitoto vidogo vya shule vinaifahamu Kenya . Kenya wameweza kujitangaza nje ya mipaka na kuna wawekezaji wengi toka nje, huku sisi tumekalia rushwa na 10 percent, unadhani mwekezaji atakuja lini? halafu Waziri husika yupo tu anakenua meno kwenye kemera. jamani tuache kuonea wivu wakenya na badala yake tujifunze mazuri toka kwao na mabaya kama yale ya kukatana mapanga tuwaachie. Mama Tibaijuka uko wapi?
 
picha nzuri sana. naona urban planners wamefanya kazi nzuri huko nairobi. siyo sawa na kwetu nyumba mtu unaijenga dizaini yako mwenyewe na unaelekeza unapotaka. hawa naona ujenzi wa nyumba zao ni uniform(zinafanana) na mji umependeza. labda pale magomeni palipokuwa nyumba za treni wakabomoa wanaweza jenga staili hizo. Hongera Nairobi.
 
Back
Top Bottom