Ndio, naelewa ya kwamba power is sweet, and the temptation to consolidate power can be really overwhelming, usifikiri Uhuru ni mtu mwema kivile, hata yeye anatamani kuwa na that authority ya Kimagufuli au Museveni.
Hata mimi 😀
In his first months in power, Uhuru alianza na fujo tu, kutoa amri hapa na pale, kufanya hili na lile bila ya kuconsult institutions zilizopo kwa mujibu wa kisheria, kelele zikawa nyingi na akapata kuaibishwa na bunge pamoja na mahakama.
Ntakupa mifano ya Anti-terrorism law na Media law ambazo alitaka kupitisha kimabavu style ya Kibaki na Moi.
Upinzani, mahakama, hasasi za raia na bunge zikampa "Red card". Akafyata.
Nchi hizi zote za EA zina serikali mithili ya kidikteta kwasababu katiba za nchi zao (ambazo wao wenyewe ndio walitunga) zimewapa mamlaka hizo, na pia raia hawahusishwi katika kutunga na kutekeleza sheria za nchi.
Katiba ya Kenya...hatusemi ni perfect, lakini wananchi wako involved sana katika uongozi wa nchi. Ili hata kubadili kipengee fulani ya katiba ni lazma wananchi kuhusishwa.