Nasikia Uhuru iko tegemea Sana hiyo tume kumpeleka Ikulu and this time itakua na members from both CORD & JUBILEE. So itakua ngumu kwake kushinda.
Hapo siwezi bisha, maana rais Uhuru kama mwanasiasa yeyote atategemea apate pa kushikilia hata kama itabidi kupindisha tume. Wanasiasa wote ni wanafiki, iwe Kenya au Tanzania hadi kule Marekani.
Lakini hilo la kusema kwamba tume ikiwa na wanasiasa member wa CORD au Jubilee eti ndio hatua muafaka ya Raila kushinda, naomba kubishana na hiyo kauli. Kwanza ufahamu hao members wote ni wachumia tumbo, hufuata mkumbo na kunusa nusa wapi hela zinakotokea. Hata hawa viongozi wa IEBC wa sasa haikutegemewa kwamba wanaweza kupinda, ikizingatiwa mwenyekiti ni mwenye asili ya Kisomali, hajatokea kwenye mikoani. Mkurungezi alikua mwenye asili ya kabila la Raila.
Nimesema tena, kwamba ushindi wa Raila utategemea pakubwa jinsi wapigaji kura wa mkoa wa magharibi watakavyompokea. Wakiamua wote kwa mpigo, hakika ataingia ikulu, lakini sio vinginevyo. Haya makelele ya IEBC anatafuta kiki tu hamna jingine. Yeye kama mwanasiasa anafahamu kwamba kwa makelele mengi na jina lake kutajwa tajwa kwenye vyombo vya habari na pia vinywani vya mamilioni ya Wakenya, kutaendelea kudumisha umaarufu wake.
Ukiangalia leo hii, makamanda wenzie akina kalonzo na Wetangula hawatajwi tajwi kama yeye, kila uchao vichwa vya habari vimekua na kauli kama hizi "Raila asema bado", "Raila atakutana na rais Uhuru", "Raila atahutubia waandishi", " "Raila asema bado hatokubali", "Raila asitisha maandamano".... yaani Raila hiki, Raila kile.... hicho ndicho chakula cha mwanasiasa.
Hivyo haya ya IEBC atatumia kila fursa kuhakikisha yamedumu, na hata yakirekebishwa, ataibukia kwengine. Juzi amealikwa ikulu na kuulizwa wazi, kinaga ubaga haswa nini kinachomsibu kwenye hili la IEBC, hapo ghafla akaanika mezani orodha kubwa ya mahitaji yake, mengine mengi hata hayahusiani na IEBC, ikiwemo uundwaji wa cheo cha waziri mkuu.
Binafsi simlaumu Raila, kama mwanasiasa lazima awe na mikakati yake ya kudumu kwenye ulingo wa siasa, kero yangu ni pale inahusu machafuko na vifo vya Wakenya.