Kenyans come this way tujadili

Kenyans come this way tujadili

Tume ya uchaguzi haipigi kura, sisi Wakenya ndio wenye kura. Kila mmoja wa viongozi atajinadi kwetu. Jukumu letu ni kuamuka asubuhi na mapema na kwenda na kutenda haki yetu ya msingi. Tume huru itakua na jukumu la kuhesabu kura.

Binafsi hapa nitakua nadanganya nikisema fulani ataibuka mshindi, maana kura yangu ni moja tu, ilhali waliojiandikisha kupiga kura ni mamilioni ya Wakenya.


My thoughts exactly!!!!


Raila needs to campaign now

Ensure most of his supporters have IDs and

Ensure he wins majority of MCAS in at least 30 counties..... Otherwise hata waeke tume ya marekani ishikilie kura hakutabadilika....


Jubilee cord nikama Remain and leave campaign za brexit hard to tell who will win


And FYI if none of the contestants achieve 50% of all votes cast plus 1 there will be a rerun in December!!
 
Nasikia Uhuru iko tegemea Sana hiyo tume kumpeleka Ikulu and this time itakua na members from both CORD & JUBILEE. So itakua ngumu kwake kushinda.

Hapo siwezi bisha, maana rais Uhuru kama mwanasiasa yeyote atategemea apate pa kushikilia hata kama itabidi kupindisha tume. Wanasiasa wote ni wanafiki, iwe Kenya au Tanzania hadi kule Marekani.

Lakini hilo la kusema kwamba tume ikiwa na wanasiasa member wa CORD au Jubilee eti ndio hatua muafaka ya Raila kushinda, naomba kubishana na hiyo kauli. Kwanza ufahamu hao members wote ni wachumia tumbo, hufuata mkumbo na kunusa nusa wapi hela zinakotokea. Hata hawa viongozi wa IEBC wa sasa haikutegemewa kwamba wanaweza kupinda, ikizingatiwa mwenyekiti ni mwenye asili ya Kisomali, hajatokea kwenye mikoani. Mkurungezi alikua mwenye asili ya kabila la Raila.

Nimesema tena, kwamba ushindi wa Raila utategemea pakubwa jinsi wapigaji kura wa mkoa wa magharibi watakavyompokea. Wakiamua wote kwa mpigo, hakika ataingia ikulu, lakini sio vinginevyo. Haya makelele ya IEBC anatafuta kiki tu hamna jingine. Yeye kama mwanasiasa anafahamu kwamba kwa makelele mengi na jina lake kutajwa tajwa kwenye vyombo vya habari na pia vinywani vya mamilioni ya Wakenya, kutaendelea kudumisha umaarufu wake.

Ukiangalia leo hii, makamanda wenzie akina kalonzo na Wetangula hawatajwi tajwi kama yeye, kila uchao vichwa vya habari vimekua na kauli kama hizi "Raila asema bado", "Raila atakutana na rais Uhuru", "Raila atahutubia waandishi", " "Raila asema bado hatokubali", "Raila asitisha maandamano".... yaani Raila hiki, Raila kile.... hicho ndicho chakula cha mwanasiasa.
Hivyo haya ya IEBC atatumia kila fursa kuhakikisha yamedumu, na hata yakirekebishwa, ataibukia kwengine. Juzi amealikwa ikulu na kuulizwa wazi, kinaga ubaga haswa nini kinachomsibu kwenye hili la IEBC, hapo ghafla akaanika mezani orodha kubwa ya mahitaji yake, mengine mengi hata hayahusiani na IEBC, ikiwemo uundwaji wa cheo cha waziri mkuu.

Binafsi simlaumu Raila, kama mwanasiasa lazima awe na mikakati yake ya kudumu kwenye ulingo wa siasa, kero yangu ni pale inahusu machafuko na vifo vya Wakenya.
 
Do you Think Mr Agwambo Raila atashinda urais after Ile TUME kuundwa upya ? Mi iko nauliza Tu na ntashukuru if nitapewa answers.
Mi mi mtanzo hiko nataka kujua Kama Ni kweli allied friend wa maghu atashinda the coming election.
Kabla sijajibu swali lako kwenye hiii hoja,ningetaka kujua mbona unatumia kiswahili kibovu hivyo?Unafanya hivyo ukikusudia au?Maanake haileti picha nzuri hata kidogo kwanza kwa mtanzania,kama kweli wewe ni mtanzania!Afu inafanya hoja yenyewe,hata kama ni hoja ya maana ionekane ya kiutaniutani na ya kipuuzi!Tokomea gizani,hata kujibu hoja yako itakuwa ni ishu!
 
Samahani mkuu . Ebu tuwe serious kujadili hoja sitoleta mzaha wa lugha tena.

Kabla sijajibu swali lako kwenye hiii hoja,ningetaka kujua mbona unatumia kiswahili kibovu hivyo?Unafanya hivyo ukikusudia au?Maanake haileti picha nzuri hata kidogo kwanza kwa mtanzania,kama kweli wewe ni mtanzania!Afu inafanya hoja yenyewe,hata kama ni hoja ya maana ionekane ya kiutaniutani na ya kipuuzi!Tokomea gizani,hata kujibu hoja yako itakuwa ni ishu!
 
Sasa mkuu what should be done Ili vita visitokee iwapo Uhuru hatambui uwepo wa upinzani na Raila naye hatambui uwepo wa rais Kenyatta. ??


[QUOTE="MK254, post: 16595720,

Binafsi simlaumu Raila, kama mwanasiasa lazima awe na mikakati yake ya kudumu kwenye ulingo wa siasa, kero yangu ni pale inahusu machafuko na vifo vya Wakenya.[/QUOTE]
 
Samahani mkuu . Ebu tuwe serious kujadili hoja sitoleta mzaha wa lugha tena.
Sawa jombaa,hamna haja ya kunajisi lugha yetu hii tukufu ya kiswahili!Kama ingekuwa ni kithungu umekitumia vibaya,ungeona wengi wanakutania.Wengine wetu hata kama ni wakenya,bado tunakienzi kiswahili.Ukiona nimetumia kiswahili kibovu nirekebishe tafadhali,tutakikuza hivo hivo tu!
 
Nimekuelewa joh pole kwa usumbufu napenda kiswahili cha hao jamaa wanapokua wanaongea .

Sawa jombaa,hamna haja ya kunajisi lugha yetu hii tukufu ya kiswahili!Kama ingekuwa ni kithungu umekitumia vibaya,ungeona wengi wanakutania.Wengine wetu hata kama ni wakenya,bado tunakienzi kiswahili.Ukiona nimetumia kiswahili kibovu nirekebishe tafadhali,tutakikuza hivo hivo tu!
 
Sasa mkuu what should be done Ili vita visitokee iwapo Uhuru hatambui uwepo wa upinzani na Raila naye hatambui uwepo wa rais Kenyatta. ??


[QUOTE="MK254, post: 16595720,

Binafsi simlaumu Raila, kama mwanasiasa lazima awe na mikakati yake ya kudumu kwenye ulingo wa siasa, kero yangu ni pale inahusu machafuko na vifo vya Wakenya.
[/QUOTE]

Vita havitotokea, na atakayepigana labda atakua mjinga wa mwisho, hawa viongozi huwa wanachumia matumbo yao tu, wanapigiana simu huko juu na kuteuana wao kwa wao na watoto wao. Mlalahoi kitaa atakua mjinga kuibuka na kumshambulia yakhe mwenzie.

Atakayeshindwa kwenye uchaguzi, akubali na kwenda kijijini kulima. Hapo nasisi itakua jukumu letu kumpa ushirikiano atayeshinda. Binafsi sitampigia kura Raila, lakini akishinda na kula kiapo cha kuwa rais wangu, nitakua nampa ushirikiano kwa lolote lile. Nitamwombea awe na hekima ili tutoke kama taifa na kupigana dhidi ya umaskini kwa kubuni ajira kwa vijana n.k.

Vivyo hivyo, Uhuru akishinda au mwengine yeyote, lazima tumkubali kama taifa. Hapa itatulazimu kuiga Tanzania, japo Magufuli ushindi wake ulikuwa wa mashaka, lakini Lowassa alikubali kutulia na kuwaacha Watanzania waendelee na maisha yao ya kawaida. Viongozi wetu wanafaa kumuiga Lowassa pakubwa, sio zile tabia zao za kusababisha machafuko kwa ajili ya kung'eng'ania madaraka.
 
Watanzania na watu wengine wasiokuwa wakenya,kwa kuaminishwa kuwa Kenya ni ukabila tu unaokithiri huwa wanaona kama siasa za Kenya zinaongozwa kwa kigezo hicho tu!Huo sio ukweli jombaa.Kama unataka kuujua uongozi wa Raila Odinga,angalia tu alivoongoza wakati alipokuwa waziri mkuu.Uongozi wake ulikuwa duni sana ukizingatia matarajio ya watu wengi waliomuunga mkono uchaguzi wa 07',mimi nikiwa mmoja wao.Ufisadi ulikithiri,sanasana upande wake,yaani kwa mawaziri aliowateua yeye kutoka kwa chama chake chini ya serikali ya muungano.Hilo si cha kusitisha zaidi ya alivowakinga na kuwatetea dhidi ya tuhuma hizo za ufisadi.Alipokosana nao,ndipo alipokumbuka kuwa wao ni wafisadi,kisha akawatema na kuwafuta kazi!Niambie kuna ubinafsi wa hali ya juu zaidi ya hiyo?Angalia anavowatumia wafuasi wake kuleta vurugu kwa minaajili ya kujiendeleza kisiasa yeye mwenyewe!Hapiganii maendeleo ya wananchi wa Kenya,anachofanya ni kuweka maslahi yake kwanza kabla ya maslahi ya wananchi wa Kenya!Ndio maana niliamua kumpigia U.Kenyatta kura '013 na hadi sasa sijajuta.U.Kenyatta hana ubaguzi wala ubinafsi na mwaka unaofata utaona wakenya wakimrudisha ikulu.Raila Odinga alipoteza nafasi alopewa na wakenya ya kujidhibitisha kuwa anatosha kama rais wa Kenya nzima na sio maeneo fulani ya kikabila!Ataiacha dunia bila kukalia kiti hicho cha urais!Hilo nina uhakika nalo!
 
Bily ,
Kwa vile avatar yako inaonesha unaipenda Tanzania, basi na mie kama jirani mwema nitachangia.

Tume ''Huru'' mpya ya Uchaguzi inategemea kama wajumbe wake watakuwa na uzalendo wa kuweka nchi mbele zaidi ya ukabila na rushwa ''kubwa kubwa''.

Somo mnaweza kuchukua toka uchaguzi wa Tume ''Huru'' Zanzibar ambapo vyama vyote vikubwa CUF na CCM walikuwa na watu wao ndani ya Tume na kuonekana ''huru'' lakini mwisho wa siku tumeona nani ameibuka ''mshindi''.

Hivyo kuwa na katiba safi katika ''karatasi'' na Tume 'Huru'' ya uchaguzi hakumaanishi kuwa mambo yatakuwa murua kama hakuna nia thabiti ya kuendesha uchaguzi ulio ''haki'' na ''huru'' na kikubwa ni hatimaye wananchi kutangaziwa matokeo yaliyo ya ''kweli''.
 
Oh sorry mkuu I'm a Tanzanian by birth ondoa shaka.

Bily ,
Kwa vile avatar yako inaonesha unaipenda Tanzania, basi na mie kama jirani mwema nitachangia.wananchi kutangaziwa matokeo yaliyo ya ''kweli''.
 
Raila atashinda uchaguzi. Ila hatopewa urais hapo ndo mziki sasa wa kiafrika. Ha ha ha ha
Maana hata wakipiga kiukabila wakelenjing na wakikuyu hawavuki 40% ya population ya kenya.
 
Do you Think Mr Agwambo Raila atashinda urais after Ile TUME kuundwa upya ? Mi iko nauliza Tu na ntashukuru if nitapewa answers.

Hili Nitakuambia for free. Huyo jamaa hawezi akashinda. In fact, atapata asilimia kidogo kushinda zile alizopata mwaka wa 2013.

Mtu asikudanganye eti kila Kitu ni Ukabila tu. Kwanini Raila na Mudavadi waligawana Kura katikati katika Jamii ya waluhya ilhali Mudavadi ni Mluhya na Raila ni Mjaluo? Mi mwenyewe ni Mluhya lakini nilimpigia Uhuru kura ilhali yeye ni mkikuyu. Tatizo hapa kuwa tu kuna viongozi ambao huwa hawana sera, na kwa hivyo, wanapenda kusema kuwa "kabila lile" au "kabila hili."
 
Watanzania achaneni na hawa wakenya...........UKABILA ni kama oxygen kwao.......haya yote wayasemayo humu ni mihemko ya kikabila tu!
Tabia hii yahitaji mabadiliko makubwa sana mioyoni mwao,kimtazamo na kisiasa pia.

none sense!
 
Watanzania achaneni na hawa wakenya...........UKABILA ni kama oxygen kwao.......haya yote wayasemayo humu ni mihemko ya kikabila tu!
Tabia hii yahitaji mabadiliko makubwa sana mioyoni mwao,kimtazamo na kisiasa pia.

none sense!

Kwanini mlitengeneza dhana kwamba kila asiyemshobokea Raila lazima atakua mkabila. Yeyote asiyempigia Raila kura ni mkabila, ili mtu asionekane mkabila lazima ampigie Raila kura. Yaani kwamba Wakenya hawana uhuru wa kufanya maamuzi ya nani wa kumpigia kura.

Huyo Raila kwanza ndiye ameendekeza ukabila pakubwa, amefunga kwa ufunguo maeneo yake hata nzi hawezi thubutu kuingia. Kila akisemacho anahakikisha kwake huko hawana uhuru wa kufanya maamuzi yao. Juzi vurugu za IEBC, kwake huko kumekua kama jehanamu, watu wanabomoa na kuchoma miundo mbinu na biashara za wawekezaji, ilhali kwa viongozi wenzie kama vile Bungoma kwa Wetangula na Kitui kwa Kalonzo hakukua na uharibifu wowote.

Mwache huo unafiki, kila Mkenya ana uhuru wa kumchagua kiongozi amtakaye, awe ametokea kwenye kabila lake au la.
 
[amefunga kwa ufunguo maeneo yake hata nzi hawezi thubutu kuingia

😀😀😀😀😀😀😀!!!
 
Back
Top Bottom