Kenyans come this way tujadili

Kenyans come this way tujadili

Kwanini mlitengeneza dhana kwamba kila asiyemshobokea Raila lazima atakua mkabila. Yeyote asiyempigia Raila kura ni mkabila, ili mtu asionekane mkabila lazima ampigie Raila kura. Yaani kwamba Wakenya hawana uhuru wa kufanya maamuzi ya nani wa kumpigia kura.

Huyo Raila kwanza ndiye ameendekeza ukabila pakubwa, amefunga kwa ufunguo maeneo yake hata nzi hawezi thubutu kuingia. Kila akisemacho anahakikisha kwake huko hawana uhuru wa kufanya maamuzi yao. Juzi vurugu za IEBC, kwake huko kumekua kama jehanamu, watu wanabomoa na kuchoma miundo mbinu na biashara za wawekezaji, ilhali kwa viongozi wenzie kama vile Bungoma kwa Wetangula na Kitui kwa Kalonzo hakukua na uharibifu wowote.

Mwache huo unafiki, kila Mkenya ana uhuru wa kumchagua kiongozi amtakaye, awe ametokea kwenye kabila lake au la.

Hivi kwanini msioane kwa kasi. Wakikuyu mvamie wanawake wa kijaluo na wajaluo hivyo hivyo. Mwisho mtakuwa na Kabila la wakenya.
 
Raila ni mkabila, Uhuru ni mkabila, vigogo wengine wote ni wakabila. Hata Magu mwenyewe mkabila. Hivyo ndivyo siasa ilivyo. Marekani na ulaya si ukabila uko bali racism(only reason Obama won, or whites always win) . Wanao wapigia kura ndo wakiwa wakabila au racist Hua kosa na taabu kwa taifa.

Hapa Kenya, lile kundi litakaloweza kushawishi eneo la magharibi kulipa kura yake asilimia tisini hivi ndilo litakaloshinda na kuingia ikulu. Ila kwa mtazamo wangu, hakuna watu wakosao ukabila Kenya hii kama wao kwani yeyote atakaye waahidi maendeleo kwa mshawishi mkubwa watampa kura. Na hio ndio demokrasia kwangu kwani hampigi kura eti juu mwenzenu agombea au jirani wako wapigia jamaa flani.

Natamani Sana wakenya wote, haswa wa hili kabila langu wawe kama waluhya kisiasa.
 
Hivi kwanini msioane kwa kasi. Wakikuyu mvamie wanawake wa kijaluo na wajaluo hivyo hivyo. Mwisho mtakuwa na Kabila la wakenya.
Sounds silly but somehow in future pple will be very integrated ...and with each passing election there are more mixed tribe pple than b4.. it MIGHT root out tribalism.
 
Hivi kwanini msioane kwa kasi. Wakikuyu mvamie wanawake wa kijaluo na wajaluo hivyo hivyo. Mwisho mtakuwa na Kabila la wakenya.

Kuoana baina ya makabila hakuwezi futa ubaguzi. Kumaliza makabila hakutamaliza ubaguzi. Dunia hii, wanasiasa bado watapata fursa ya kutugawa kimakundi hata kama tukiongea lugha moja. Somalia wote dini moja, lugha moja lakini kutwa wanauana na kubaguana.

Hata hiyo Bongo, wengi tunajua mnavyobaguana kimya kimya, kiukanda, kidini, kichama, kijinsia, hata kiukabila japo sio sana kama Kenya n.k.
Ubaguzi upo dunia yote. Cha msingi ni watu kubadilika kimtazamo, unafaa kumuona mwenzio kama binadamu anayefaa. tatizo huwa pale wanasiasa wanakua wanafiki, yeye anakua wa kwanza kuelekeza kidole cha lawama kwa wenzie lakini kwake mbaguzi wa hali ya juu.

Leo hii ukithubutu kutoendana na rais Uhuru kwake mkoa wa kati, au uthubutu kumpinga Raila kwenye mikoa yake ya Nyanza, ndio utajua kilichomsibu mtema kuni. Mijitu inatokwa na povu na kukushambulia. Lakini hao hao viongozi watataka dunia iwaelewe kuwa wao ndio safi kabisa na hawana ukabila.
 
Ni kweli ubaguzi upo dunia nzima na hauwezi kuisha, lakini kinachofanyika ni kupunguza risks zinazotokana na ubaguzi ambazo zawezwa kuwa triggered na wanasiasa.
Mfano mkioana kwa kasi, ubaguzi utabakia kwenye mambo ya siasa tu hautaleta mambo makubwa hasi kwa jamii kwa ujumla. Lakini mkiendelea kuishi kwa mfano, rift valey ni wa kalejing tu na wanaona wakalejing tu na ukienda Kisumu ni wajaluo tu wanaoa wajaluo tu. ukienda huko juu ni wapokot tu wanaoana kipokot tu.

Hali hiyo inatengeneza mazingira mazuri ya sio racism tu ya ukabila , bali ya mauaji na uhasama ulio na mizizi mizuri na sawia. Maana mjaluo anafahamu kabisa nikipeleka polisi kwa wapokot watauliwa wapokot chansi ya kuuawa mjaluo ni infinitely small. In turn however, inajenga mazingira ya chuki na uhasama na kujiapiza .
Kenya kilichopo sio racism(ubaguzi) ya kikabila wala kikanda bali imeshakwisha vuka mipaka na imeshakuwa uhasama kwa maoni yangu. Unaweza uficha huu uhasama kwa koti la ubaguzi wa kabila. Lakini ukweli ni uhasama ambao umejengwa kwa misingi ya hizi jamii kutoingilia ktk kasi stahiki.
 
Before it seemed to be so obvious,but now no one can say who will win...and it is too early to even get to such a conversation,because both leaders are okay in the eyes of many,a 50/50 thing. So personally am more concerned with 2022. This is just a race to quench both of the leaders thirst
My two cents. 2017 was to be a walk in the park for Jubilee. Things have changed. I think if CORD could have RAO as kingmaker to someone else, then it is a walk in the park for them. If RAO insists on being the candidate then it will go to a run-off because in the absence of the ICC cases in 2017, there wont be much to comeout and vote for especially in the rift valley. A run off is like a penalty shoot out, highest turn out wins.
 
Ni kweli ubaguzi upo dunia nzima na hauwezi kuisha, lakini kinachofanyika ni kupunguza risks zinazotokana na ubaguzi ambazo zawezwa kuwa triggered na wanasiasa.
Mfano mkioana kwa kasi, ubaguzi utabakia kwenye mambo ya siasa tu hautaleta mambo makubwa hasi kwa jamii kwa ujumla. Lakini mkiendelea kuishi kwa mfano, rift valey ni wa kalejing tu na wanaona wakalejing tu na ukienda Kisumu ni wajaluo tu wanaoa wajaluo tu. ukienda huko juu ni wapokot tu wanaoana kipokot tu.

Hali hiyo inatengeneza mazingira mazuri ya sio racism tu ya ukabila , bali ya mauaji na uhasama ulio na mizizi mizuri na sawia. Maana mjaluo anafahamu kabisa nikipeleka polisi kwa wapokot watauliwa wapokot chansi ya kuuawa mjaluo ni infinitely small. In turn however, inajenga mazingira ya chuki na uhasama na kujiapiza .
Kenya kilichopo sio racism(ubaguzi) ya kikabila wala kikanda bali imeshakwisha vuka mipaka na imeshakuwa uhasama kwa maoni yangu. Unaweza uficha huu uhasama kwa koti la ubaguzi wa kabila. Lakini ukweli ni uhasama ambao umejengwa kwa misingi ya hizi jamii kutoingilia ktk kasi stahiki.

Binafsi bado hilo la kuoana kusudi tumalize ukabila bado haliniingii. Watu huoana kwa ajili wanapendana, kijana anamchumbia msichana aliyempenda halafu mengine yanakua historia. Lakini eti ulazimishe vijana waoe kutoka kwenye makabila tofauti ukitegemea ndio utamaliza ukabila, hilo halina msingi.

Nyerere alijaribu kufanya hilo kwenu lakini nina uhakika hiyo haikua suluhu. Tanzania kilichowasaidia ni kwamba, nchi iliongozwa na mtu wa kutokea kwa kabila ndogo hapo mwanzo. Mzanaki wa kutokea Butiama akajikuta Dar es Salaam eti anaongoza nchi, halafu hao Wazanaki sidhani hata kama ungewahesabu Dar, wasingetimia hata mia. Lakini kama mngethubutu kuongozwa na mtu wa kutokea kabila kubwa kwa mfano Wachagga, ndio mngekoma kuanzia hapo mwanzo. Leo hii hiyo Tanzania yenu bado unakuta hayo makabila makubwa wameajiriana wao kwa wao kwenye nyadhifa muhimu (hutendeka japo kimya kimya).

Kenya kilichotuponza ni nchi kuongozwa na mtu wa kutokea kabila kubwa hapo mwanzo, akaendekeza mfumo wa watu kuona jinsi ya kujitoa ni kuhakikisha anayeongoza nchi ametokea kwa kabila lako. Kuanzia hapo pakaibuka ushindani baina ya makabila. Wakati ukweli wa mambo ni kwamba hamna siku rais atakusaidia hata kama ametokea kwa kabila lako. Mimi binafsi ni Mkikuyu, kabila ambalo limefaulu kutoa marais watatu nchini, lakini hamna hata siku moja nimefaulu kufanya jambo lolote kisa rais wangu Mkikuyu, mishe zangu kila siku nimehangaika mwenyewe kwa bidii yangu.

Nimekatiza mikoa mingi hadi hata Bongo, nikihangaika mwenyewe, hajanisaidia rais yeyote. Lakini itachukua muda mrefu kuondoa hiyo dhana kwa Wakenya, maana ilipandwa pale mwanzo, halafu wanasiasa wamefaulu kuwadanganya watu wao kwamba fursa zao zimebanwa na uongozi uliopo kwa kutumia makabila yanayoongoza. Halafu pia marais wenyewe hawajafaulu kufuta hiyo dhana, maana kila wakiteua, unakuta majina ya wateule wengi ni ya watu wa kutokea kwenye makabila yao. Hata kama wachache, lakini hilo linalea na kukuza hiyo dhana kwamba rais yupo kwa ajili ya watu wa kabila lake.

Lakini bado nasimamia pale, kwamba hauwezi kumaliza ukabila kwa kuzima makabila. Watu wataendelea kuishi kwenye maeneo yao na kuoana baina yao. Hata Bongo, leo hii hutategemea kuwakuta Wakwere wamejaa Bukoba, bali utawakuta kwao maeneo ya Bagamoyo, na Wahaya kwao Bukoba. Labda mmoja mmoja tu ndiye utapata kasafiri kutoka hayo maeneo. Hata Dar ambapo ni mji mkuu, lakini kuna maeneo ukienda utakuta watu wameitana na kuishi wa kabila moja. Hebu nenda maeneo ya Mbezi, Kimara utanielewa.

Suluhu Kenya ni ile siku tutachagua kiongozi kutokea kabila ndogo, hapo Wakenya watajua kumbe sio lazima rais awe wa kabila lako ndio utoke kimaisha. Leo hii ushindani upo baina ya makabila makubwa pekee yao.
 
Nakubaliana na hoja zako zote, hasa uliposema Rais kamwe hawezi kuleta maendeleo ya individuals. Aidha, mtu individual ya mpasa kufanya kazi tu ili kupata maendeleo yake. Na pia nakubaliana nawe ya kwamba Rais kazi yake ni kuleta ile kitu inayoitwa fair playing ground, yani ya kwamba hakuna corruption wala kujuana ktk kufanikisha jambo la mhusika, bali weledi wa mhusika ndo muamuzi. Hiyo nayo ni kweli tupu.

Ila bado nasimama kwa point yangu, ya kwamba tatizo la kenya sio ukabila ni uhasama. Na huo uhasama ili uushe hakuna budi kuichanganya jamii kwa kuoana na kuachana na mambo ya jamii.

Mfano Tanzania, wanapopigana wakulima na wafugaji hawapigani kwa msingi ya kabila yani ya kwamba wafugaji wakimasai na kisukuma wanenda kupigana na wakulima wa kimasai na kisukuma. Ni mapigano ya kimasilahi sio uhasama yani ya kuwa huyu mkulima anaweza acha ukulima akawa mfugaji akijiunga na kundi lile alilopigana nalo awali.

Kwa upande wa Kenya, ni uhasma wapokot wanapigana na waturkana regardless what, the moment you stand in their way, umekwisha. Hawa wanapigana kwa sababu za kijamii za uhasama. the same applies kwa wajaluo na wakikuyu hawa watu wana uhasama kama tu wa waturkana na wapokot.
Sema ugomvi wa kikuyu na wajaluo upo wame u mordenize ktk koti la siasa. Ila kiuhalisia sio siasa wala ukabila hawa watu wana uhasama linahitajika jicho pevu yenye mboni sahihi kuliona hilo.

Wakalenjing wao hawana uhasama sana sana wana flip flop kulingana na mazingira. Na kama wakenya wote mngekuwa kama wakelenjing ama kabila la Mudavadi (waluya if not mistaken) ama wakamba. Basi ni kweli solution ingekuwa rais kutoka kabila dogo. Ila ilivyo kwa sasa siamini ktk hilo. Research question yenu yapaswa kuwa muumalize je uhasama uliopo na sio kuumaliza ukabila uliopo.
 
Nakubaliana na hoja zako zote, hasa uliposema Rais kamwe hawezi kuleta maendeleo ya individuals. Aidha, mtu individual ya mpasa kufanya kazi tu ili kupata maendeleo yake. Na pia nakubaliana nawe ya kwamba Rais kazi yake ni kuleta ile kitu inayoitwa fair playing ground, yani ya kwamba hakuna corruption wala kujuana ktk kufanikisha jambo la mhusika, bali weledi wa mhusika ndo muamuzi. Hiyo nayo ni kweli tupu.

Ila bado nasimama kwa point yangu, ya kwamba tatizo la kenya sio ukabila ni uhasama. Na huo uhasama ili uushe hakuna budi kuichanganya jamii kwa kuoana na kuachana na mambo ya jamii.

Mfano Tanzania, wanapopigana wakulima na wafugaji hawapigani kwa msingi ya kabila yani ya kwamba wafugaji wakimasai na kisukuma wanenda kupigana na wakulima wa kimasai na kisukuma. Ni mapigano ya kimasilahi sio uhasama yani ya kuwa huyu mkulima anaweza acha ukulima akawa mfugaji akijiunga na kundi lile alilopigana nalo awali.

Kwa upande wa Kenya, ni uhasma wapokot wanapigana na waturkana regardless what, the moment you stand in their way, umekwisha. Hawa wanapigana kwa sababu za kijamii za uhasama. the same applies kwa wajaluo na wakikuyu hawa watu wana uhasama kama tu wa waturkana na wapokot.
Sema ugomvi wa kikuyu na wajaluo upo wame u mordenize ktk koti la siasa. Ila kiuhalisia sio siasa wala ukabila hawa watu wana uhasama linahitajika jicho pevu yenye mboni sahihi kuliona hilo.

Wakalenjing wao hawana uhasama sana sana wana flip flop kulingana na mazingira. Na kama wakenya wote mngekuwa kama wakelenjing ama kabila la Mudavadi (waluya if not mistaken) ama wakamba. Basi ni kweli solution ingekuwa rais kutoka kabila dogo. Ila ilivyo kwa sasa siamini ktk hilo.

Kaka labda ingekua bora utumie muda wako zaidi kuelewa ugomvi baina ya jamii Kenya na dunia. Hamna cha uhasama wala nini, tatizo lipo pale pale kuhusu raslimali, kama ilivyo baina ya wakulima na wafugaji Tanzania. Ukiangalia kila ugomvi Kenya, unahusiana na raslimali, halafu wanasiasa kiaina wanajua jinsi ya kupamba.

Hao hao Wapokot na Waturkana wanapigana na kuibiana ng'ombe, Mturkana au Mpokot hakurupuki kumvamia mwenzie bila sababu eti kisa amemchukia. Na ndio maana siku hizi hayo mambo yanaendelea kupuguzwa maana wengi wamejikita kwenye ukulima wa mazao badala ua mifugo. Hapo wavamizi wanakosa cha kuja na kuiba.

Mjini, Wakikuyu na Wajaluo wanaishi pamoja kwa miaka kwenye mitaa ya Kibera, wanataniana kila siku, na kula pamoja, kuuziana bidhaa kama mandugu na majirani. Lakini ikifikia wakati wa uchaguzi tu, wanasiasa huwa wanajua wapi pakubonyeza. Wanawahubiria chuki zinazohusu raslimali, mara ooh watu wa kabila hili wakichukua uongozi, raslimali zenu zitaisha, mara ooh sisi watu wa kabila hili tukiongoza, mali yote hii itakua yetu.

Ukienda kule kwa Wakalenjin, hali ni hiyo hiyo ya raslimali. Hawakurupuki kuvamia kisa wanawachukia wenzao, maana siku zote wanaishi pamoja tu, vurugu huibuka pale tunapofikia kwenye uchaguzi. Na ndio maana nikasema, nchi ikiongozwa na mtu neutral, wa kati, asiyetokea kwenye baina ya haya makabila makubwa, labda wa kabila ndogo Pwani, huu ushindani utapungua. Watu wataona kumbe sio rais wa nchi ndiye anayesababisha raslimali ziongezeke au kupungua ndani ya kabila fulani.

Raslimali ndio huwa chanzo cha ugomvi duniani, soma historia. Hata hiyo Bongo, raslimali zikipungua, utaanza kuyaskia tu. Leo hii mna visa vichache maana raslimali zipo, haswa ardhi ni kubwa. Jamaa yangu hapo Mtanzania huko kijijini, alipewa shamba kwa uwezo wa kurusha jiwe. Yaani alipewa kajiwe kadogo akaambiwa arushe na pale litakapotua, ndio mwisho wa shamba lake. Umeskia wapi mambo kama hayo, yaani ardhi bado nyingi na bikira. Raslimali, hususan ardhi ndio husababisha haya yote unayoyaskia duniani.
 
Nakubaliana na wewe.
Sasa uchaguzi ujao mmepe Mdavadi ama kama vipi mkubaliane wanaloleta vurugu ktk uchaguzi ni wakikuyu, wajaluo na Kalejing. Wapigeni ban kugombea urais kwa miaka 10. Hapo uone povu litakavyowatoka hayo makabila.
 
Hilo haliwezekani, viongozi waliopo kwenye frontline ndio hao wanaoongoza hayo makabila makubwa, na wamefaulu kuyatia mifukoni. Leo hii utawaambia nini Wakikuyu kwamba Uhuru hafai, au utumie ujuzi gani kuwakanya Wajaluo dhidi ya Raila. Ukithubutu, utaishia hospitalini au kaburini.

Tutaenda vivyo hivyo tu hadi mwisho, maana hamna namna, labda vizazi vya baadaye saana. Cha msingi ni kiongozi ajaye, hata kama wa kabila kubwa, ajaribu juu chini kupunguza umaskini na kuinua kiwango cha elimu ili watu waweze kujiinua kimaisha, mengine hayo hayatakua na umuhimu.

Leo hii wanaopiga kura sana kwa mihemuko ya kikabila ni walalahoi mitaani, maana hao wameaminishwa akiingia kiongozi fulani, basi umaskini kwao umeisha. lakini umaskini ukipungua, huo ushindani utapungua, na wanasiasa wengi wanalifahamu hilo, na ndi maana huwa hawapendi watu wa maeneo yao wakielimika au kuboreka kimaisha, kusudi waishi wakiwa maskini na kuwa wategemezi kiakili.
 
Yah apo kwenye kwenye maandish mekundu ni kweli mtupu hata hapa bongo hivi vitu vipo sana na nimeviona wengi ni sababu ya umasikini na ukosefu wa elimu unachangia kwa kiwango kikubwa sana
 
Back
Top Bottom