Kaka labda ingekua bora utumie muda wako zaidi kuelewa ugomvi baina ya jamii Kenya na dunia. Hamna cha uhasama wala nini, tatizo lipo pale pale kuhusu raslimali, kama ilivyo baina ya wakulima na wafugaji Tanzania. Ukiangalia kila ugomvi Kenya, unahusiana na raslimali, halafu wanasiasa kiaina wanajua jinsi ya kupamba.
Hao hao Wapokot na Waturkana wanapigana na kuibiana ng'ombe, Mturkana au Mpokot hakurupuki kumvamia mwenzie bila sababu eti kisa amemchukia. Na ndio maana siku hizi hayo mambo yanaendelea kupuguzwa maana wengi wamejikita kwenye ukulima wa mazao badala ua mifugo. Hapo wavamizi wanakosa cha kuja na kuiba.
Mjini, Wakikuyu na Wajaluo wanaishi pamoja kwa miaka kwenye mitaa ya Kibera, wanataniana kila siku, na kula pamoja, kuuziana bidhaa kama mandugu na majirani. Lakini ikifikia wakati wa uchaguzi tu, wanasiasa huwa wanajua wapi pakubonyeza. Wanawahubiria chuki zinazohusu raslimali, mara ooh watu wa kabila hili wakichukua uongozi, raslimali zenu zitaisha, mara ooh sisi watu wa kabila hili tukiongoza, mali yote hii itakua yetu.
Ukienda kule kwa Wakalenjin, hali ni hiyo hiyo ya raslimali. Hawakurupuki kuvamia kisa wanawachukia wenzao, maana siku zote wanaishi pamoja tu, vurugu huibuka pale tunapofikia kwenye uchaguzi. Na ndio maana nikasema, nchi ikiongozwa na mtu neutral, wa kati, asiyetokea kwenye baina ya haya makabila makubwa, labda wa kabila ndogo Pwani, huu ushindani utapungua. Watu wataona kumbe sio rais wa nchi ndiye anayesababisha raslimali ziongezeke au kupungua ndani ya kabila fulani.
Raslimali ndio huwa chanzo cha ugomvi duniani, soma historia. Hata hiyo Bongo, raslimali zikipungua, utaanza kuyaskia tu. Leo hii mna visa vichache maana raslimali zipo, haswa ardhi ni kubwa. Jamaa yangu hapo Mtanzania huko kijijini, alipewa shamba kwa uwezo wa kurusha jiwe. Yaani alipewa kajiwe kadogo akaambiwa arushe na pale litakapotua, ndio mwisho wa shamba lake. Umeskia wapi mambo kama hayo, yaani ardhi bado nyingi na bikira. Raslimali, hususan ardhi ndio husababisha haya yote unayoyaskia duniani.