Baado Tanzania tuna safari ndefu,angalia mambo CCm inayoyafanya kwa kuvunja sheria,inatumia magari ya serikali,mawaziri wake bado wako ofisini na wakati huohuo wako kwenye kampeni,wanaagiza mabango toka Canada na halipii ushuru,
Ndio maana sikuhangaika kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura,kwani hakuna lolote litakaloweza kufanywa kwa kutumia haki yangu ya kupiga kura bila ya kubadilisha katiba,na nimeapa kama katiba haitabadilishwa sitajiandikisha kupiga kura hadi kaburini,mambo yanayofanyika sasa hapa nchini kwetu ni kuchezeana akili,hebu angalia mtu anaweka pingamizi la hovyo ili apite bure kisa eti jina limekosewa herufi.Mfano hai ni wa Waziri Masha,alivyokuwa anampigia simu mgombea kupitia Chadema,na hao ndio viongozi vijana tunaowategemea watufikishe Kanaani kwenye nchi ya asali na maziwa!.Kwa mara ingine hongereni Wakenya mmejitofautisha na nchi zote za EAC,kama Uganda ambako M7 anang'ang'ania madaraka,Rwanda kwa dikteta Kagama na Burundi ambako kote huko mambo ni hovyo hovyo.