joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Ninampango wa kuhama hili jukwaa la Kenya siku za karibu, sitoendelea kuchangia kwasababu ya kiwango kidogo cha uwelewa wa mambo mnachokionyesha ninyi wakenya, haina maana kama mtu anatoa comment bila kuifanyia utafiti wa kina, Miradi yote mnayoipoteza sababu kubwa sio Tanzania.Kusema ukweli, Rwanda ni nchi huru na wanahaki ya kubadilisha akili yao kuhusu mambo kama haya. Wakiamua kujiunga na Sgr ya Tanzania, pia ni sawa. Tunawaombea Wanyarwanda kila la kheri. Tanzania mumejaribu sana kutuny'ang'anya miradi yetu lakini haina shida. Bado tunazidi kupepea na Sgr yetu lazima ikamilike. Kumbuka miradi nyingi ya T.Z bado haijaanza au ndio tu imeanza kwa hivyo don't count your chicks before they hatch. Kenya itazidi kutamba ukanda huu na hatuendi kokote.
Rwanda ilikua tayari kuunganisha na Kenya, lakini Uganda ilisema haitokuwa na uwezo wa kujenga vipande vitatu kwa wakati mmoja, hivyo walichagua kuchagua Kampala kwenda Juba badala ya Kigali kutokana na ukubwa wa biashara kuwa mkubwa kuliko ule wa Rwanda na Uganda, Rwanda haikua na choice nyingine zaidi ya kuigeukia Tanzania, je Tanzania inahusikaje katika hilo?