Kenyatta, Arap, Kibaki, Kenyatta, Arap - huu ukiritimba wa Uongozi ndio hayati Magufuli alipambana kuufuta!

Makabila mengine ni marufuku kuwa Rais Kenya. Mjaluo anaweza ongoza America na sio kuongoza Kenya. Rais Kenya anawekwa na ukubwa wa kabila lake na sio ubora wake
 
Labda aache leo ufisadi,je atapambana na ufisadi bila kuacha ufisadi?
 
... kama ilivyo Kiswahili, bin/binti, "arap" ni neno la Kikalenjin (anakotokea Dr. Ruto) likiwa na maana hiyo hiyo ya bin sawasawa na Kimasai "ole" kwa mwanaume.

William arap Ruto ni sawa tu na ungemwita William bin Ruto. Hana uhusiano wa kifamilia na Moi zaidi ya kuwa kabila moja.
 
1. Ali H. Mwinyi
2. Husein Mwinyi
3. Jakaya Kikwete
4. Ridhwan Kikwete
5. Kinana namsikia toka nipo primary
6. Makamba Jr
7. Makamba Sr
8. Nnauye Sr
9. Nnauye Jr
10. List ni ndefu sana

"Toa kwanza boriti kwenye jicho lako.."
LUka 6:41-45
George Bush senior-George bush jr
Bill Clinton-Hillaly Clinton
 
Hata Raila Odinga baba yake Jaramogi Oginga Odinga alikuwa Makamu wa Rais Kenya.

Kwa hivyo, kama unakataa dynasties, Ruto ndiye mtu ambaye hakuwa na kiongozi katika familia yake.
 
Huu uchaguzi was about issues na ndo maana wakikuyu wengi wamempatia kura Ruto.. ni mojawapo ya uchaguzi ambao haukuwa na mrengo wa ukabila na ukanda.. sasa sijui hii narrative yako umeitolea wapi mkuu
 
Mwanzo wa kabila ni nini?
 
Hata Raila Odinga baba yake Jaramogi Oginga Odinga alikuwa Makamu wa Rais Kenya.

Kwa hivyo, kama unakataa dynasties, Ruto ndiye mtu ambaye hakuwa na kiongozi katika familia yake.
Kama Mkapa!
 
Nani alifuta Magufuli? Huyu aliyetaka kuondoa term limit?
 
Kenya kuna Arap Kirwa, Arap Ruto, Arap Sae Lakini wote hawana undugu na Arap Moi.
 
Nadhani picha inaongea..All four presidents of Kenya in one pic,hapo ndipo utapata relationship
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…