usinisogeze
Senior Member
- May 6, 2017
- 199
- 122
You guys, the constitutional gives power the president to do any thing. Kwa hiyo Dogo hayo yote anayoyafanya ni kwa mujibu wa katiba inayompa mamlaka hayo.Katiba peke yake bila utashi wa kisiasa si kitu,hapa kwetu katiba inatoa uhuru wa mawazo,mikutano na maandamano,mbona vyote vimezuiwa kwa amri kutoka juu? Rais Kenyatta angekuwa na hulka ya kidikteta hakuna chombo chochote kingeweza kumzuia,yeye ndiye mkuu wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama,angeweza kutoa amri ya kuwaswaga kama kuku wale wote ambao wangeleta fyokofyoko,lakini kwa sababu ya kutanguliza uzalendo wake,hakuona sababu ya kumwaga damu za Wakenya ili abaki madarakani,amekuwa mnyenyekevu na mtii kwa Taifa lake kuliko kujivunia vyeo.
Hapa kwetu mtu kuongea ukweli tu anaitwa mchochezi,sasa hivi kuna makosa mapya kabisa yamedownloadiwa na vyombo vya dola,nayo ni kumsema rais hadharani.Tundu Lissu alikamatwa kwa kosa la kumsema rais hadharani,kwamba hakupaswa kuusema ukweli juu ya kushikiliwa kwa ndege yetu,alipaswa apige kimya! Sasa kama mtu anadiliki kuwakamata wanaomkosoa huku katiba ikiruhusu ukosoaji,kwa nini msiitwe madikteta?
Kumfananisha Rais Kenyatta na miungu watu yenu ni uhayawani wa kiwango cha lami!Kenyatta ni mdemokrasia,mzalendo na mcha Mungu,anastahili pongezi,yeye ndiye alama ya sababu za kusifiwa kwa demokrasia ya Kenya,angekuwa mbinafsi leo hii tungekuwa tumeshawapokea Wakenya kama wakimbizi.
Sent using Jamii Forums mobile app