Kenyatta si Mwanademokrasia ila Katiba ya Kenya ni ya Kidemokrasia

Kenyatta si Mwanademokrasia ila Katiba ya Kenya ni ya Kidemokrasia

Katiba peke yake bila utashi wa kisiasa si kitu,hapa kwetu katiba inatoa uhuru wa mawazo,mikutano na maandamano,mbona vyote vimezuiwa kwa amri kutoka juu? Rais Kenyatta angekuwa na hulka ya kidikteta hakuna chombo chochote kingeweza kumzuia,yeye ndiye mkuu wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama,angeweza kutoa amri ya kuwaswaga kama kuku wale wote ambao wangeleta fyokofyoko,lakini kwa sababu ya kutanguliza uzalendo wake,hakuona sababu ya kumwaga damu za Wakenya ili abaki madarakani,amekuwa mnyenyekevu na mtii kwa Taifa lake kuliko kujivunia vyeo.

Hapa kwetu mtu kuongea ukweli tu anaitwa mchochezi,sasa hivi kuna makosa mapya kabisa yamedownloadiwa na vyombo vya dola,nayo ni kumsema rais hadharani.Tundu Lissu alikamatwa kwa kosa la kumsema rais hadharani,kwamba hakupaswa kuusema ukweli juu ya kushikiliwa kwa ndege yetu,alipaswa apige kimya! Sasa kama mtu anadiliki kuwakamata wanaomkosoa huku katiba ikiruhusu ukosoaji,kwa nini msiitwe madikteta?

Kumfananisha Rais Kenyatta na miungu watu yenu ni uhayawani wa kiwango cha lami!Kenyatta ni mdemokrasia,mzalendo na mcha Mungu,anastahili pongezi,yeye ndiye alama ya sababu za kusifiwa kwa demokrasia ya Kenya,angekuwa mbinafsi leo hii tungekuwa tumeshawapokea Wakenya kama wakimbizi.
You guys, the constitutional gives power the president to do any thing. Kwa hiyo Dogo hayo yote anayoyafanya ni kwa mujibu wa katiba inayompa mamlaka hayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali ni, Tz ni katiba ndio ya kidikteta au ni ni yule nani? Anaitwaje tena.....
 
Katiba inamruhusu Mkuu kufanya hayo ingawa wengine walishindwa kufanya hayo kwa uoga wao. Nyerere alihawi sema hilo, ingawa sisi tumewekeza zaidi ya kumjadili rais badala ya mapinduzi ya mfumo.
Swali ni, huko tz ni katiba ndo ya kidekta au ni ni ule nani?
 
Katiba inamruhusu Mkuu kufanya hayo ingawa wengine walishindwa kufanya hayo kwa uoga wao. Nyerere alihawi sema hilo, ingawa sisi tumewekeza zaidi ya kumjadili rais badala ya mapinduzi ya mfumo.

katiba inamruhusu kuvunja katiba?!!
 
pic+kenya.jpg


Nimejaribu kufuatilia sana purukushani za uchaguzi wa Kenya mpaka sasa. Nimesoma haya:

1. Katiba ya Kenya ni zuri sana na haijatoa mwanya wa mtu kujiinua;

2. Kenyatta anaroho ya kutokubali demokrasia ila anafungwa na Katiba. Natolea mfano wa matamushi aliyotoa juu ya wale walioamua kesi ya uchaguzi. Amewaita kwa maneno mengi sana. Ila kubwa ni lile alilosema ni "wakora". Sina maana kamili kwa kiswahili cha kwetu, ila naamini anamaanisha wanyang'anyi. Ameendelea kusema kuwa majaji wote waliompigia kura za kuopinga uchanguzi wamefanya maamuzi hayo kisiasa. Hili ni kweli? Ni jambo la kujiuliza.

Kwa sababu hiyo, leo Chama cha Mawakili nchini Kenya (LSK) kimemkosoa Rais Uhuru Kenyatta baada ya kuwashambulia majaji wa mahakama ya juu kufuatia uamuzi wa kubatilisha uchaguzi wake.

Rais wa LSK Isaac Okero alimkosoa Rais Kenyatta kwa kumtaja Jaji Mkuu David Maraga na majaji wengine wa mahakama hiyo kuwa wamekosea.

Okero amesema Matamshi ya rais kwamba majaji hao wasubiri rais achaguliwe katika uchaguzi ujao hayafai kutoka kwa kiongozi wa taifa ambaye chini ya katiba ya Kenya ni nembo ya umoja wa Wakenya.

Wewe unasemaje hapo? Kenyatta ni mwanademokrasia au ni Katiba imemfunga?
Hii mada yako makes no sense. Ni kama kusema "USA is a nation of rule of law " lakini ukiangalia ndio unapata wao wana wafungwa milioni mbili sasa hivyo wao sio watu wa sheria.
 
Mbona hata hapa katiba ipo lkn mara kadha wa kadha inavunjwa? Angalia wanakataza uhuru wa watu kutoa maoni hata wa kujumuika, wakati katiba inaruhusu!

Hivyo hata Uhuru angeweza tu kukiuka katiba lkn hajafanya hivyo.
 
Haya sasa ameanza kutoa makucha yake ya Kiafrika. Katiba inabadilishwa rasmi kumpitisha kuwa sultani.
Hii mada yako makes no sense. Ni kama kusema "USA is a nation of rule of law " lakini ukiangalia ndio unapata wao wana wafungwa milioni mbili sasa hivyo wao sio watu wa sheria.
 
Kama kumbukumbu zangu ziko sawa, Mwaafrika pekee nnayemjua kama MWANADEMOKRASIA ni MANDELA tu (RIP). Kama kuna mwingine mniambie!
 
Kuna wengi wamepiga debe tupu kwa Kenyatta. Wengine tunaopenda kufiri tukaonekana tunashabikia
Kama kumbukumbu zangu ziko sawa, Mwaafrika pekee nnayemjua kama MWANADEMOKRASIA ni MANDELA tu (RIP). Kama kuna mwingine mniambie!
 
Kama kumbukumbu zangu ziko sawa, Mwaafrika pekee nnayemjua kama MWANADEMOKRASIA ni MANDELA tu (RIP). Kama kuna mwingine mniambie!
Leopold Cedar Sengor (Senegal); Jerry J.Rawlings (Ghana); Ahmadou Ahijo (Cameroon); Quet Massire (Botswana); Siakka Stevens (Sierra Leone); Joachim Chissano (Mozambique); Julius Nyerere (Tanzania); Sam Nuyoma (Namibia) nk, wapo sio kwamba hawapo.
 
Back
Top Bottom