KERO: Baadhi ya Walimu wa boarding sio waaminifu

Kelela

Senior Member
Joined
Nov 7, 2020
Posts
191
Reaction score
308
Kama mupo walimu wa tabia hii jirekebisheni.

Mzazi unahangaika unapata chochote kitu unaamua kumtumia mwanao pesa ya matumizi, kwa kuwa wanafunzi hawaruhusiwi kumiliki simu tunatumia namba zenu walimu kama munavyotuambia.

Sasa baadhi ya walimu hamna uaminifu, unatumiwa pesa ya mtoto na unakubali kabisa na kusema unamjua ila ukitumiwa pesa haumpatii mtoto. Mtoto anaendelea kupata shida wakati pesa alishatumiwa na mzazi wake. Hii tabia inakera na sio uungwana.

Hii imenikuta, mwalimu kabla hujamtumia hela anakuwa mchangamfu sana kukujibu, ukishamtumia tu anaona tabu hata kujibu sms zako.

KAMA MSHAHARA HAUTOSHI ANZISHENI MIRADI SIO KUTEGEMEA PESA ZA MATUMIZI ZA WANAFUNZI, MUNAKATILI WATOTO.
 
Sasa umekuja kulalamika hapa ili iweje?

Si ungeenda kwenye hiyo shule ukalalamike

Maana hapa haitasaidia
 
Najua hii tabia haipo shule moja, Nimetoa uzi huu kama tahadhari kwa wengine.

Kuhusu ilo lililonikuta mimi ninalifuatilia kwenye shule husika.

Ila huu uzi nimetoa kwa lengo la kuelimisha.
 
Mwalimu asije akaniletea huo upuuzi anaweza akasababisha nikachukua sheria mkononi.
 
Sasa umekuja kulalamika hapa ili iweje?

Si ungeenda kwenye hiyo shule ukalalamike

Maana hapa haitasaidia
Kiherehere cha kuwa wa kwanza kuandika!! [emoji848] Kama huhusiki siyo lazima kujibu. Humu ni sehemu ya watu wengi, ujumbe wake unaweza kuponya wengi.
 
Wewe na mwanao wote viraza wakubwa.

Unashndwaje kufungua akaunti ya benki ukawa unamtupia huko kila ukipata senti na mwanao anafuata kila apatapo muda?

Siku hizi kila kona hadi vijajini kuna mawakala wa mabenki.

Mawasiliano ya mwanafunz na mzaz yote yapitie kwa mkuu wa shule, makam wake, mwalimu wa malez na patron/matron.

Nawapongeza walimu wenzangu mnaowapa adabu wazaz vilaza ingawa wajuaji na endeleeni.
 
Wewe hujielewi, na ni miongoni mwa matapeli, unafikiri kila shule ipo mjini. Shule ipo km kadhaa kutoka mjini, kwa hiyo afunge safari ya masaa manne kwa ajili ya kutoa ela, na shule hawaruhusu mwanafunzi kutoka tu kiholela nje ya shule, pesa ya matumizi wanataka zitumwe kwa walimu. Au Haujasoma Boarding itakuwa.
 
Pole, hili swala ni kweli lipo kwa baadhi ya walimu wasiowaaminifu Kama ulivyosema ila haya pia yanachangiwa na baadhi ya wazazi kwani baadhi hawataki kupitia njia rasmi zilizowekwa na shule husika, kwa mfano. Shule inataka pesa na mawasiliano yote vipitie kwa mwl wa malezi ila mwanafunzi hataki kwani anaona ni usumbufu kutumia simu moja kwa wote hivyo anampa mzazi namba ya mwl. Mwingine asiyehusika na swala hilo.

Pili mzazi anatuma pesa tena kwa wakala hasemi kisa tu aliongea na mwl. Juzi, shule ina wanafunzi zaidi ya 900 kwa mfano htajuaje pesa ya nani? So mwl Kama sio mwaminifu ataipiga tu, kumbe hata ukiamua kumtumia pesa mtumia jina la mwanafunzi, kidato ikibidi na tahasusi yake.

Vilevile baadhi ya wazazi sio wasataarabu , mke wangu alikuja kulia kwangu kwamba Kuna mtoto Hana nauli na shule amefunga kwao hajaenda miaka miwili mzazi wake anaomba akopeshwe Tsh 50,000/ Kama nauli ya mtoto....ilienda na maji
 
Na bado, tutawapiga sana hivyo vielfu 20 vyenu.
Mnataka sie tukale wapi?
 
Kama mupo walimu wa tabia hii jirekebisheni.

Mzazi unahangaika unapata chochote kitu unaamua kumtumia mwanao pesa ya matumizi, kwa kuwa wanafunzi hawaruhusiwi kumiliki simu tunatumia namba zenu walimu kama munavyotuambia.

Sasa baadhi ya walimu hamna uaminifu, unatumiwa pesa ya mtoto na unakubali kabisa na kusema unamjua ila ukitumiwa pesa haumpatii mtoto. Mtoto anaendelea kupata shida wakati pesa alishatumiwa na mzazi wake. Hii tabia inakera na sio uungwana.

Hii imenikuta, mwalimu kabla hujamtumia hela anakuwa mchangamfu sana kukujibu, ukishamtumia tu anaona tabu hata kujibu sms zako.

KAMA MSHAHARA HAUTOSHI ANZISHENI MIRADI SIO KUTEGEMEA PESA ZA MATUMIZI ZA WANAFUNZI, MUNAKATILI WATOTO.
Bado hawajaanzisha pre 1,prep 2, naseri graduu kila party laki tano ama milioni moja.
Mara michango ya mtihani.
Yaani Kama Hawa walimu wetu wanakera. Waziri amekataa watoto wasisome Ila wao wanahangaika kukodi chumba mbali wasome kimya kimya kisa eti la Saba. Miaka yote Saba ama sita mlikuwa wapi kutowandaa watoto mnakuja kukomaa dakika za lala salama
 
Na bado, tutawapiga sana hivyo vielfu 20 vyenu.
Mnataka sie tukale wapi?
Shame on you!
Yaani mwalimu unashadadia kuiba, sasa nini maana ya kuwa mwalimu. Au una ulimbukeni na Ualimu.
Ndio maana vijana wakitoka shule wanakuwa na tabia za hovyo, kuna baadhi ya walimu kama nyinyi ndio munawaharibu.
 
Unamtumia mwanao kila siku hela lakini anayemfikishia mwanao hela hujawahi kumtumia hata buku. Wazazi na walezi muwe mnawajali walimu.
 
Kwa uzoefu wangu shule nyingi kama sio zote zina utaratibu wa kuhifadhi pocket money za wanafunzi aidha kwa mhasibu, matron au mkuu wa shule ili kuepusha kuibiana bwenini
Lakini tatizo ni wazazi wengi kuwa na akili ngumu na kusikiliza watoto wao kwamba ukimpa mwl ataipata haraka na bila kuhojiwa hojiwa.
 
Shame on you!
Yaani mwalimu unashadadia kuiba, sasa nini maana ya kuwa mwalimu. Au una ulimbukeni na Ualimu.
Ndio maana vijana wakitoka shule wanakuwa na tabia za hovyo, kuna baadhi ya walimu kama nyinyi ndio munawaharibu.
Tulia wewe mzazi na sisi tufaidi mema ya nchi.
 
Kama mupo walimu wa tabia hii jirekebisheni.

Mzazi unahangaika unapata chochote kitu unaamua kumtumia mwanao pesa ya matumizi, kwa kuwa wanafunzi hawaruhusiwi kumiliki simu tunatumia namba zenu walimu kama munavyotuambia.

Sasa baadhi ya walimu hamna uaminifu, unatumiwa pesa ya mtoto na unakubali kabisa na kusema unamjua ila ukitumiwa pesa haumpatii mtoto. Mtoto anaendelea kupata shida wakati pesa alishatumiwa na mzazi wake. Hii tabia inakera na sio uungwana.

Hii imenikuta, mwalimu kabla hujamtumia hela anakuwa mchangamfu sana kukujibu, ukishamtumia tu anaona tabu hata kujibu sms zako.

KAMA MSHAHARA HAUTOSHI ANZISHENI MIRADI SIO KUTEGEMEA PESA ZA MATUMIZI ZA WANAFUNZI, MUNAKATILI WATOTO.
Mtoto yupo boarding school, wewe unamtumia hela ya nini? kwani hapo shuleni hakuna kitu gani? Sera ya shule inasemaje? Unavunja sheriaa halafu unalalamikia huku, fata taratibu kama hiyo shule haikidhi hadhi yako hamisha mwanao!!!
 
Kwa sisi wazazi wenye watoto na tunao jua thamani ya watoto wetu ametusaidia
Thamani ya mtoto kwa kumtumia hela kwa njia haramu? unamfundisha mtoto tabia gani hapo!! Kwa shule zenye utaratibu huo hela zinawekwa dukani yeye anatumia daftari lake kama kitabu cha benki!!
 
Wewe hujielewi, na ni miongoni mwa matapeli, unafikiri kila shule ipo mjini. Shule ipo km kadhaa kutoka mjini, kwa hiyo afunge safari ya masaa manne kwa ajili ya kutoa ela, na shule hawaruhusu mwanafunzi kutoka tu kiholela nje ya shule, pesa ya matumizi wanataka zitumwe kwa walimu. Au Haujasoma Boarding itakuwa.
Kwahiyo mwalimu ndio afunge safari akakutolee pesa ya mwanao? Ulimpa na nauli?
 
Shame on you!
Yaani mwalimu unashadadia kuiba, sasa nini maana ya kuwa mwalimu. Au una ulimbukeni na Ualimu.
Ndio maana vijana wakitoka shule wanakuwa na tabia za hovyo, kuna baadhi ya walimu kama nyinyi ndio munawaharibu.
Hapo ewe Mzazi au Mlezi wa mtoto unapotea, fata sheria inavyoelekeza na hili haliwezi kukutokea, Kumbuka unamfundisha mwanao tabia mbaya, na huko sio kumpenda mtoto! Kama shule haikidhi viwango vyako, hamisha mwanao,,,full stop vinginevy kaa kimya
 
Back
Top Bottom