KERO Kero foleni Mlimani City, Dar

KERO Kero foleni Mlimani City, Dar

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kuna njia mbadala.

1. Unaweza kupita Mawasiliano (Terminal) Road ukaingia Sinza Mugabe then ukaenda zako aidha kupita Barabara ya Tandale Hadi Kawawa Road then Ally Hassan Mwinyi.

2. Pita Morogoro Road then Shekilango halafu Bagamoyo Road.

Foleni inaweza ikawa inasababishwa na dereva kutokujua njia mbadala.
Umeandika as if una uhakika mwenzako anaendesha usafiri wake binafsi anaweza akabadili njia. Labda yupo kwenye daladala na mahali anapotokea daladala zinapita hapo
 
Foleni mlimani City ni kero.

Kila asubuhi Traffic huongoza magari upande hasa yanayotokea Goba/UDSM kupita na kusababisha foleni kubwa kwa magari yanayotoka Ubungo.

Foleni unaweza kukaa mpaka nusu saa wakati kuna round about ilipaswa kupunguza foleni.

Ni kero kubwa inayosababisha wengi wetu kuchelewa makazini.
Mpaka treni za chini ya ardhi ziwekwe ndio foleni itakwisha Dar. Lakini akili hii sio ya CCM!
 
Umeandika as if una uhakika mwenzako anaendesha usafiri wake binafsi anaweza akabadili njia. Labda yupo kwenye daladala na mahali anapotokea daladala zinapita hapo
Aisee ni kweli nilivyokuwa ninaandika nilisahau kwamba Kuna watu hawana usafiri binafsi.

Kero za usafiri zilinifanya ninunue usafiri mdogo. Kwa Sasa ninasafiri njia niipendayo.
 
Huwa wanafunga junction kabisa. Hakuna anaeenda wanabaki kulaumiana.
Sio madereva kabisa hawa, ukiwaachia kidogo tu hamna gari inapita, afadhari daladala huwa wanaongea na kuachiana nafasi wapite. Gari ndogo kila mmoja kapandisha kioo juu na mziki/redio wala hasikii chochote kapoa tu.
 
Kuanzia Ubungo hadi Mwenge ilitakiwa ijengwe barabara ya juu ili kuondoa foleni
 
Back
Top Bottom