Kero gani huwa unapata mtandao wa intanet ukikosekana eneo ulilopo?

Kero gani huwa unapata mtandao wa intanet ukikosekana eneo ulilopo?

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Kuna maeneo ukienda kupata mtandao inakuwa kipengele sana, mtandao haushiki na ukishika ni kwa kuutafuta mpaka unatamani kulia, kama ni wa kuperuzi sana unashindwa kama ni mtu wa kufanya kazi mtandaoni ndio hali inakuwa ngumu.

Mawasiliano pia inakuwa changamoto kwa yale yanaohitaji mtandao moja kwa moja, mpaka unajiuliza hawa watu huku wanaishije kwa ulimwengu huu tulipofika ambao fursa nyingi ziko mtandaoni.

Tuambie kukosekana kwa mtandao kumewahi kukupa hasara gani na ulikuwa wapi?
 
Mimi kila ikifika saa 3 usiku et mtandao unapungua kasi, hadi inanilazimu nibadilishe line tu! ........yani inakera sana mkuu....
 
Mimi kila ikifika saa 3 usiku et mtandao unapungua kasi, hadi inanilazimu nibadilishe line tu! ........yani inakera sana mkuu....
Bora Upungue Kasi Yapo Maeneo Kyerwa, Ngara Oops
Mtandao Haupatikani Roaming Na Hakuna Kupiga, Sms Haziendi
 
Back
Top Bottom