KERO KUU ZA BIASHARA TANZANIA: Wageni kufanyabiashara sawa na wazawa, Polisi kugeuka maafisa Kodi, TRA kushindwa kutengeneza mazingira halisi ya Kodi

KERO KUU ZA BIASHARA TANZANIA: Wageni kufanyabiashara sawa na wazawa, Polisi kugeuka maafisa Kodi, TRA kushindwa kutengeneza mazingira halisi ya Kodi

Street Hustler

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
2,175
Reaction score
4,299
Naona wafanyabiashara wanashindwa au wanasau kero kuu za Biashara pale Kariakoo.

1. Kuwaruhusu Wachina watoke China waje kuchuuza Biashara zao hapa TANZANIA na kariakoo WACHINA wenyewe wanakopeshana na wanapeana mali kwabei nafuu tofauti na mtanzania anaenda kununua bidhaa China alafu hapo hapo wewe mtanzania huruhusiwi kufanya biadhara hapo China, Sasa inakuwaje sie Tanzania tunawaruhusu Wachina na wageni kuja kufanya Biashara hapa Tanzania kwanini hao wageni wasifanye Biashara za kuanzisha viwanda kuliko kufanya uchuuz pale kariakoo.

Hili nalo linaenda sambamba na Biashara ya mazao kwanini serikali imemruhusu mgen hasa wakenya na waganda kwenda shambani kununua mazao kwa mkulima kwanini serikali isiwadhibiti hao walanguz wakutane sokoni hasa mazao ya mahindi, maharage, viazi, kitunguu, nyanya na vinginevyo.

2. Kero nyingine Ni Hawa Askari Kiukweli Hawa wamekuwa kero kiuhalisia hamna wanachofanya zaidi ya kukulazimisha uwape rushwa Sasa anakusimamisha unampa risiti anasema hyo thamani sio yeye anajua sio anaduka wapi usipofanya wanavyotaka unaingia kwenye matatizo yaan Askari wote hao wapikipiki, wamagari na wale kwenye mageti barabarani.

3. Kodi na malipo yamekuwa mengi sana kwanini huo mrundikano usilipiwe kwenye leseni manispaa pili kwann bidhaa isilipiwe Kodi bandarini nahuku mtaan mtu kusiwe na usumbufu, nafkiri TRA walitakiwa kukadiria full ili mtu ajue analipa Mara moja na anakuwa huru kufanya Biashara yake.

Hz Mambo za TBS, TMDA, fire, usafi, ulinzi, mwenge na nyingine Basi zilipiwe kwenye leseni watazikuta halmashauri kuruhusu na kuwaoa nafasi watu kupita madukan n kutengeneza mazingira ya rushwa.
 
Uzi kama hizi zenye mambo ya msingi hawataki kuchangia pumbavu kabisa

Umeandika vizuri sana
Wanataka kuchangia zile za Amina na abdala kichwa Waz, lakin hyo ndio tafsir ya vijana wataifa hili ambao hawataki kufanya ya msingi ili wale Bali wanataka kufanya vya rahis na kipuuz na jion wale kitu ambacho hakiwezekani kwenye dunia yasasa.
 
Tanzania itapata maendeleo endelevu na ya kweli pale ambapo wananchi (wafanyabiashara, wakulima na wafanyakazi wenye uzoefu kwenye sekta binafsi) watakapokuwa wengi kwenye nafasi za maamuzi au madaraka.
Huu ulegevu wa kuacha nchi inakuwa shamba la bibi kwa wageni unatokana na fikra potofu, kukosa ufahamu wa kihalisia kwa watumishi wengi wa serikali na viongozi (practice makes perfect). Mtu yeyote ambaye hajapambana uraiani, ambaye mapato yake ni rushwa na hisani hawezi kuwa kiongozi mzuri wa kuwasaidia wananchi.
Mara nyingi viongozi, vyombo vya dola na hata mahakama wana fikra za kitumwa za kusaidia wageni kwa dhana potofu ya kukarbisha wawekezaji.
Uwekezaji lazima uwe kwa faida ya wananchi na taifa kwa ujumla na siyo vinginevyo.
 
Mada nzuri ila wachangiaji ni wachache maana ujinga wa middle class ndio mtaji wa watawala, President Nyerere yote haya aliyaona na kwa makusudi mazima akaamua kuyafagilia chini ya zuria, sio kuyazoa na kutupa nje, nchi hadi leo haina taasisi imara zenye kujitegemea ambazo zingesaidia utawala bora, angalia Botswana why wao wamemudu kuwa na taasisi imara, na inashangaza sana Marais wa kwanza wa nchi hizi wote wamesomea England!,wote wanarudi kwenye nchi zao na kuwa Marais, ila nchi hizi zinachukua uelekeo tofauti kabisa, why Tanzania tuwe na 60M ya watu ,Botswana less than 3M,why tumezaana sana kuliko uwezo wa kutunza watoto hawa?,why police wetu ni rushwa mno, vibaraka wa politicians, hawalindi nchi bali status ago ya royal families?,tatizo la kariakoo ni matokeo ya uozo mkubwa toka huko nyuma
 
Unamkuta Polisi yupo busy kusoma Karatasi ya kutoa mzigo ya TRA ambayo hajui hata kimoja kilichoandikwa humo muda mwingine vimiminika vinaandikwa kwa ujazo wake kwa Ujumla yeye anatafuta sehemu iliyoandikwa idadi ya box haipati mimi huwa wakiniuliza nawaambia mkuu tafuteni mimi hata sijui kama ninyi na mnawezaje kufanya kazi ya kitu msichokijua...wanabaki kusema unajifanya lijuaji Mkuu...nachekaa maana najua hawajui kitu kweli mwisho utasikia tupe ya maji basi nawaambia nishalipa kodi wazee wao hawapendi kuona umenyooka wanatafuta dili kwa nguvu...
 
Tanzania itapata maendeleo endelevu na ya kweli pale ambapo wananchi (wafanyabiashara, wakulima na wafanyakazi wenye uzoefu kwenye sekta binafsi) watakapokuwa wengi kwenye nafasi za maamuzi au madaraka.
Huu ulegevu wa kuacha nchi inakuwa shamba la bibi kwa wageni unatokana na fikra potofu, kukosa ufahamu wa kihalisia kwa watumishi wengi wa serikali na viongozi (practice makes perfect). Mtu yeyote ambaye hajapambana uraiani, ambaye mapato yake ni rushwa na hisani hawezi kuwa kiongozi mzuri wa kuwasaidia wananchi.
Mara nyingi viongozi, vyombo vya dola na hata mahakama wana fikra za kitumwa za kusaidia wageni kwa dhana potofu ya kukarbisha wawekezaji.
Uwekezaji lazima uwe kwa faida ya wananchi na taifa kwa ujumla na siyo vinginevyo.
Hizi nafasi natamani Sana vijana tulioko kwenywe mitaa ndio tunaojua Taifa linataka nn umegusa sehemu nyeti Sana private sector Kuna watu productive sana naamini Kuna ka mstar kadogo tuu wakaruhu na kesho ya Neema ifunguke
 
Mada nzuri ila wachangiaji ni wachache maana ujinga wa middle class ndio mtaji wa watawala, President Nyerere yote haya aliyaona na kwa makusudi mazima akaamua kuyafagilia chini ya zuria, sio kuyazoa na kutupa nje, nchi hadi leo haina taasisi imara zenye kujitegemea ambazo zingesaidia utawala bora, angalia Botswana why wao wamemudu kuwa na taasisi imara, na inashangaza sana Marais wa kwanza wa nchi hizi wote wamesomea England!,wote wanarudi kwenye nchi zao na kuwa Marais, ila nchi hizi zinachukua uelekeo tofauti kabisa, why Tanzania tuwe na 60M ya watu ,Botswana less than 3M,why tumezaana sana kuliko uwezo wa kutunza watoto hawa?,why police wetu ni rushwa mno, vibaraka wa politicians, hawalindi nchi bali status ago ya royal families?,tatizo la kariakoo ni matokeo ya uozo mkubwa toka huko nyuma
Hili Taifa kuna watu waliamua either kwakujua au kwa kutokujua huwez kuruhusu kila mikutano wako wa siasa bongo muvi/fleva wawepo hapa ndio shida Leo huku mtaan yaan Bibi ,mama, na mjukuu wanagombea remote waangalie season/tamthilia
 
Mada nzuri ila wachangiaji ni wachache maana ujinga wa middle class ndio mtaji wa watawala, President Nyerere yote haya aliyaona na kwa makusudi mazima akaamua kuyafagilia chini ya zuria, sio kuyazoa na kutupa nje, nchi hadi leo haina taasisi imara zenye kujitegemea ambazo zingesaidia utawala bora, angalia Botswana why wao wamemudu kuwa na taasisi imara, na inashangaza sana Marais wa kwanza wa nchi hizi wote wamesomea England!,wote wanarudi kwenye nchi zao na kuwa Marais, ila nchi hizi zinachukua uelekeo tofauti kabisa, why Tanzania tuwe na 60M ya watu ,Botswana less than 3M,why tumezaana sana kuliko uwezo wa kutunza watoto hawa?,why police wetu ni rushwa mno, vibaraka wa politicians, hawalindi nchi bali status ago ya royal families?,tatizo la kariakoo ni matokeo ya uozo mkubwa toka huko nyuma

Taasisi imara huundwa na watu imara.
Watu wenye upeo mpana kwanza, mengine kama taasisi na hata taifa imara yatatokea automatically.
Usitegemee kuwa na serikali, bunge au mahakama imara kama watumishi/wahusika au watendaji wake siyo imara.
 
Ulikuwa ni ujinga, na hata sasa makosa yanarudiwa rudiwa.

Ukijenga nyumba yenye misingi mibovu nyufa zikuwa zikitoke kila mara.
Na unakuta jumba limejaa viraka vya nyufa na nyufa mpya. Miaka nenda rudi, wako "busy" kuziba nyufa tu - Kumbe tatizo liko kwenye msingi.

Unapopata nafasi ya kujenga nyumba mpya, hakikisha unaanza kwa "kuplan" vya kutosha na kujenga msingi imara. Nafasi hii waliipata kina Nyerere, na wakaaharibu. Na sasa legacy yake ni baba wa taifa bovu.

Sasa, mambo ya kuanza kuboma nyumba iliyokamilika, ili kuijenga mpya kwa kuanzia na msingi imara ni GHARAMA sana. Kwa Tanganyika hii gharama haiepukiki, kama nia ni kutatua chanzo cha tatizo.

Lakini pia, ukiachana na gharama, kuna uwezekano mkubwa, wakazi wa hiyo nyumba wa baadae, wasijue kwanini inapata nyufa mara kwa mara, au wakajua chanzo cha tatizo, lakini wajanja wachache wanaonufaika na hilo tatizo, wakahakikisha nyumba haibomolewi ili kujengwa upya - Matokeo ni kuziba nyufa, juu ya nyufa.

Pole sana Tanganyika.
 
Back
Top Bottom