KERO Kero kwenye vivuko, Dar es Salaam

KERO Kero kwenye vivuko, Dar es Salaam

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

The useful idiot

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2024
Posts
1,019
Reaction score
2,670
Hawa watu wa vivukoni ni bora wafurushwe wote kuanzia anaesafisha vyoo hadi wasimamizi!! Hii ni total failure, vivuko vyote vimeharibiwa kimebaki kimoja mara kwa mara kinazimika njiani!

Tulizoea huduma ni Masaa 24 ila kwa sasa huduma inaishia saa nane usiku!! Leo kwenye kuscan kadi upande wa posta mashine moja tu ilikua zinafanya kazi na kupelekea msongamano wa watu!!

Ni bora serikali iangalie namna ya kuboresha huduma kwenye vivuko hii ni aibu kubwa sana, hata Bakhresa naamini akipewa asimamie hapo mambo yataenda vizuri kabisa.

Ni kitu gani serikali imeweza kusimamia na kuleta mafanikio?? Labda kwenye Tozo tu, ndio maana daraja la kigamboni linaenda vizuri.

NB : serikali haimaanishi ni Mama Samia, bali hao wanaoteuliwa ndio wanamkwamisha Raisi wetu.

JamiiForums ephen_ Palina FaizaFoxy
 
Back
Top Bottom