lugendo_einstein
Member
- Jul 13, 2024
- 5
- 3
Naomba kuwasilisha kero kwa Mamlaka zinazohusika kwani madarasa ya Shule ya Sekondari Teule ya Kigoma Ujiji katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji yanavuja jambo linalowapa shida Wanafunzi.
Wakati mvua zinaponyesha kunakosekana utulivu wa kusoma kwakuwa kila mahali panakuwa panavuja, hali hiyo pia inachangia hata Walimu kusitisha mchakato wa masomo kwa kuwa kila mtu anakuwa katika kujiweka katika nafasi nzuri kukwepa kulowana.
Natoa wito Uongozi wa Shule urekebishe suala hili, ni jambo dogo lakini linakera na linasababisha usumbufu mkubwa kwa Walimu na Wanafunzi.