Kero: Muwe mnawanyoa wake zenu wakikaribia kujifungua

Daktari au Nesi mwenye maadili anayeheshimu na kuipenda kazi yake hawezi kuposti ujinga kama huu sababu ni jukumu lao kutoa elimu ya afya kwa mama anayetarajiwa kujifungua.

Ujauzito au mimba unabebwa kwa miezi tisa ambayo mama na mwenza wake watahudhuria kliniki. Kama mama hajazingatia usafi maana yake wanaohusika na kutoa elimu wakati wa kliniki hawajatimiza wajibu wao.

Katika kipindi cha mahudhurio ya kliniki mama na mwenza watapimwa na kupata elimu ya afya na kujiandaa na uzazi unaokuja.


Wamama wajawazito wa siku hizi wapo vizuri na wasafi. Hata vijijini wajawazito wakienda kliniki wanapendeza ni sehemu yao ya mtoko (out fulani).

Namuheshimu sana nakumpenda mwanamke ila namuheshimu zaidi mwanamke mjamzito anayebeba mimba na kujifungua.

Heshima kwenu kwa wanawake wote mliojaliwa kubeba ujauzito na kuendelea kuijaza Dunia.

Ulimwengu ndio mama na bila nyinyi hakuna ulimwengu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…