Kero na changamoto za kwenye magroup ya WhatsApp

Kero na changamoto za kwenye magroup ya WhatsApp

KikulachoChako

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2013
Posts
19,185
Reaction score
37,239
Habari za mida hiii wadau.

Maendeleo ya kiteknolojia yameleta unafuu wa maisha na kuyafurahia maisha hasa kwenye mawasiliano.

Lakini maendeleo hayo kwa upande mwingine yameleta usumbufu na kero hasa yakikutana ndugu zetu ambao hawana nidhamu kwenye kutumia.

Kumekuwa na makundi ya kupiga soga kupitia mtandao wa WhatsApp.

Ni jambo zuri lakini limekosa muongozo kwa kuwa mara nyingi waunganishaji au waongozaji hawaangalii au kuzingatia maudhui ya kundi lao, wao kazi yao ni kuunganisha tu.

Unajikuta umeungwa kwenye huku ikifuatiwa mamia ya jumbe mbali mbali za majadiliano kwenye kundi hilo.

Simu inakuwa haina utulivu kila muda zinaingia jumbe mbali mbali, hata unashindwa kuzingatia mambo yako ya msingi.

Wewe umekumbana au unakumbana na kero gani kwenye haya makundi ya kupiga soga.
 
Maisha ya magroup ya WhatsApp nilishayaacha siku nyingi

Nilikuja kugundua group la WhatsApp linaweza hata kugombanisha familia na ukoo..

Mmejazana wanaukoo huko ni kusemana tu inbox huko..
 
Habari za mida hiii wadau........

Maendeleo ya kiteknolojia yameleta unafuu wa maisha na kuyafurahia maisha hasa kwenye mawasiliano...........

Lakini maendeleo hayo kwa upande mwingine yameleta usumbufu na kero hasa yakikutana ndugu zetu ambao hawana nidhamu kwenye kutumia........

Kumekuwa na makundi ya kupiga soga kupitia mtandao wa WhatsApp......

Ni jambo zuri lakini limekosa muongozo kwa kuwa mara nyingi waunganishaji au waongozaji hawaangalii au kuzingatia maudhui ya kundi lao......wao kazi yao ni kuunganisha tu.........

Unajikuta umeungwa kwenye huku ikifuatiwa mamia ya jumbe mbali mbali za majadiliano kwenye kundi hilo...........

Simu inakuwa haina utulivu kila muda zinaingia jumbe mbali mbali.......hata unashindwa kuzingatia mambo yako ya msingi.....

Wewe umekumbana au unakumbana na kero gani kwenye haya makundi ya kupiga soga.....
Kila kitu kina faida na hasara zake.
Ukiona Kundi uliloungwa linakuletea shida basi unaweza ukajiondoa.
 
Maisha ya magroup ya WhatsApp nilishayaacha siku nyingi

Nilikuja kugundua group la WhatsApp linaweza hata kugombanisha familia na ukoo..

Mmejazana wanaukoo huko ni kusemana tu inbox huko..
Kuna group tuki nalo tulianzisha kwa nia ya kusaidiana kwenye shida tuna miaka miwili tuna kiasi cha 16m tunafikiria kuanzisha kampuni au uwekezaji.
 
Ukiona gruop hulielewei unajitoa ukishindwa kujiondoa una mute group unakua hupati notification yoyote. Halafu pia kuna setting za kufanya mtu asiweze kuku add kwenye group bila ridhaa yako.
 
Jumbe zinazotumwa katika makundi haya ya WhatsApp nyingine zina changamoto kubwa sana. Hivi karibuni kuna katibu wa jumuiya katika kanisa letu alituma "clip" ya ngono, Toka mwaka 2024 uanze hajaudhuria tena katika jumuiya.

Siku zote alijitoa sana na kukemea dhambi hasa zinaa. Jumuiya nzima tulimuona ni mtu mwenye hofu ya Mungu mpaka tukamchagua kuwa kiongozi wetu.
 
Wale wapumbavu" samahani kwa kuingia inbox lengo langu tuwe tunaview status nikusave nani" hawa wanatokana na magroup
 
Kuna group tuki nalo tulianzisha kwa nia ya kusaidiana kwenye shida tuna miaka miwili tuna kiasi cha 16m tunafikiria kuanzisha kampuni au uwekezaji.
Subiri apatikane wa kuzila, kwanza hilo group ni la ukoo au la watu mnafahamiana au mmekutana humohumo?
 
Group la Elimu ,lakini mtu anatangaza biashara ya karanga😭
 
Habari za mida hiii wadau.

Maendeleo ya kiteknolojia yameleta unafuu wa maisha na kuyafurahia maisha hasa kwenye mawasiliano.

Lakini maendeleo hayo kwa upande mwingine yameleta usumbufu na kero hasa yakikutana ndugu zetu ambao hawana nidhamu kwenye kutumia.

Kumekuwa na makundi ya kupiga soga kupitia mtandao wa WhatsApp.

Ni jambo zuri lakini limekosa muongozo kwa kuwa mara nyingi waunganishaji au waongozaji hawaangalii au kuzingatia maudhui ya kundi lao, wao kazi yao ni kuunganisha tu.

Unajikuta umeungwa kwenye huku ikifuatiwa mamia ya jumbe mbali mbali za majadiliano kwenye kundi hilo.

Simu inakuwa haina utulivu kila muda zinaingia jumbe mbali mbali, hata unashindwa kuzingatia mambo yako ya msingi.

Wewe umekumbana au unakumbana na kero gani kwenye haya makundi ya kupiga soga.
Kulikuwa na group la shule ya secondary yaani wao muda wote ngono ni story
 
Back
Top Bottom