Kero uwanja wa Benjamini W. Mkapa! Hali ni mbaya

Kero uwanja wa Benjamini W. Mkapa! Hali ni mbaya

Freyzem

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2013
Posts
10,120
Reaction score
24,667
Tff na Wizara ya michezo kwa ujumla pamoja na wahusika wengine wote akiwemo meneja wa uwanja, hili liwafikie!

Kiukweli uwanja wa Taifa unatia aibu sana, miundombinu imechakaa, viti vimechakaa vingine vimeng'oka, vingine vimepauka yaani kwenye majukwaa kwa kweli hali ni mbaya!

Uwanja huu ambao ulipewa jina la Benjamini Willium Mkapa ulizinduliwa mwaka 2007, na hadi hivi sasa ni takribani miaka 14 imekwisha pita na cha kushangaza viti vilivyowekwa tokea 2007 hadi leo hii ndio vilivyopo uwanjani!

Viti hivyo asilimia kubwa vimeshaisha muda wake ikilinganishwa na hali ya joto la Dar es salaam yaani vimeshalihimili jua hadi kiwango cha mwisho!

Kuhusu kwenye pitch wanajitahidi sana kukuza na kuzilinda nyasi ili majukwaani kwa kweli imezidi!

Haiingii akilini mtu analipa tiketi ya VIP lakini akifika kule anakuta kiti kinatobo katikati, au kimepasuka!

Hii ni aibu hata wageni wanaoingia pale huwa wanashangaa sana!

Mapato ambayo yamekwishaingizwa pale taifa ni makubwa sana na bado yanazidi kuingia, na vile vile serikali inatenga bajeti katika wizara ya michezo, isitoshe TFF inapokea fungu kutoka FIFA kwa ajili ya kuendeleza michezo ni kwa nini katika hayo mafungu kisitengwe kiasi kwa ajili ya kurekebisha miundombinu ya huo uwanja?

Hakika katika hili wadau na wapenda michezo yafaa kuhakikisha tunalisemea ili marekebisho yafanyike na uwe wa kisasa zaidi!

Zaidi pia miundombinu ya vyoo nayo haiko sawa, vyoo vingine vimeziba maji hakuna wakati mwingine yaani huko vyooni kunatia kichefuchefu!

Tff na serikali kwa ujumla msikazanie tu masuala ya mikataba ya gsm huko na clubs, tupieni macho pia kwenye huu uwanja mkubwa kabisa hapa Afrika mashariki ambao kwa sasa unaanza kuoza baadhi ya maeneo kabla haujaoza zaidi! Bado hamjachelewa...
 
wahusika wanajali mnapopatupia macho tu (pitch),hawajui mashabiki wakifungwa dakika za mwisho huacha kutazama mpira na kuanza kutazama viti walivyokalia na kuhudhuria uani mara mbili mbili.
 
TFF ya hovyo na ya mchongo,utachukuaje % ktk kila mechi halafu hufanyi marekebisho?

Hakuna kitu kibaya kama umebanwa na mkojo unaenda kukojoa kwenye vyoo vya uwanjani pale unakuta mikojo imejaa kama mafuriko hata pa kukanyaga hakuna na maji hayatoki..

Kwa sisi wengine wenye mioyo dhaifu mkojo huwa unakata wenyewe MTU unarudi tena kumalizia mechi utoke utafute njia mbadala.

Hii ni aibu kwa kwakweli,Ustaarabu kwa wabongo umekuwa msamiati mgumu sana kueleweka na hili LA kutofanyia ukarabati linaongezea watu kutokuwa wastaarabu kwa sababu MTU akikuta maji hakuna or mifereji ya kusafirisha haja ndogo imeziba anaunga tu hajiulizi Mara mbili.

Walau kukiwa kusafi MTU anaona aibu ya kufanya Ujinga wake kama yule shabiki mwenzangu wa Yanga juzi kwenye mechi na Simba video yake ilikuwa inasambaa mitandaoni akikamatwa akiwa analimwaga kojo uwanjani.

Yaani vyoo vipo ila MTU haendi kujisaidia vyooni anaamua kujisaidia eneo ambalo watu wanakaa.Ajabu sana.
 
Tff na wizara ya michezo kwa ujumla pamoja na wahusika wengine wote akiwemo meneja wa uwanja, hili liwafikie!
Kiukweli uwanja wa Taifa unatia aibu sana, miundombinu imechakaa, viti vimechakaa vingine vimeng'oka, vingine vimepauka yaani kwenye majukwaa kwa kweli hali ni mbaya...
Huo uwanja ni wa Serikali kwa maana ya Wizara ya michezo na utamaduni, nashangaa tangu 2007 wanapata pesa kutokana mgao wa viingilio uwanja umeanza kuharibika hata Pitch yake haifai kwasasa, Wizara ilione hilo ifanye marekebisho haraka pesa wanayo
 
Sijui huwa tunakwama wapi kufanya maintenance ya vitu. Daraja la nyerere nalo tumeshindwa kurudishia zile taa.
Tatizo la maintenance kwa sekta ya umma ni kuwa bajeti mpaka mwaka Hadi mwaka na inaweza isikubaliwe. Uwanja ingekuwa ni Mali ya mtu au kampuni, boss anatoa maamuzi on the spot, kitu kinafanyika.
 
Na club nazo zijitahidi ziwe na viwanja vyao.
Huo uchezewe mechi maalum tu.
Kuna wale jamaa Wana Jenga uwanja wao kigamboni sijui wamefikia wapi?[emoji16][emoji16]

Naunga mkono hoja ya clubs kuwa na viwanja vyake! Ufinyu wa viwanja ndio unaowafanya hao mabwana wanaohusika na uwanja wa taifa wajione miungu watu na kuuacha uoze...
 
Kuna kipindi viti vilipauka sana kwa jua nikaona mtu anavipulizia moto hivi vikabadilika tena rangi mkoleo[emoji23][emoji23] ndio michezo yao

Kwa kweli hiyo ishu hata mie nilishai observe, hata kama ndiyo teknolojia inayotumika kuvihuisha, huwezi fanya hivyo kwa kiti cha miaka zaidi ya 10 aiseeh!
 
Back
Top Bottom