Kero: Wafanyakazi wa UDART kituo cha Kimara mwisho muache kukwaruzana na wateja (wasafiri)

Kero: Wafanyakazi wa UDART kituo cha Kimara mwisho muache kukwaruzana na wateja (wasafiri)

luangalila

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2014
Posts
6,346
Reaction score
6,928
Kumezuka ka tabia hawa wakatisha tiketi wa Udart na wale.wanao scan na kuchana .zile tiketi kurushiana maneno na wateja kwa maana wanao safiri

Leo pale kimara mwisho majira ya saa kumi jioni ktk folen ya kuelekea Kibaha kijana.mmoja.mchana tiketi alikuwa ana rushiana maneno na msafiri.mmoja mwanamama mjamzito , walikwaruzana sanaa yule mama.mjamzito , yule kijana akawa ana.waambia wafanyakazi wenzake huyu "dada haniambii kitu mimi na deal na watu hawa siku nzimaaaa "

Kiukweli wanapaswa waelewe ya kuwa ile ni huduma na lzm waangalie na kujali lugha nzuri unapo.zungumza na mteja ,.
Ukiachana na kisa cha leo, jana pia majira kama ya leo brother mmoja wa makamo.kidogo.pia alizozana sanaa na mkatisha tiketi za kidirisha cha kwenda Mbezi , yule mkatisha tiketi alimuita yule brother "chizi" kisa chao kilikuwa ni tiketi ambayo jamaa alinunua ktk icho kidirisha then alipokwenda ku scan ikabainia ime expire walizozana sanaa

Yule mkatisha tiketi akajifanya kumuita wale walinzi wao wa kampuni ya China -Tanzania nikawaacha hapo katika mzozo kisa tiketi

Sasa kwa tabia hizi ambazo zimejitokeza kwa hawa baadhi ya wafanya kazi wa Udart hasa idara ya wakatisha tiketi na wanao scan tiketi katika kituo cha KIMARA MWISHO ni vyema ikadhibitiwa na uongozi wa udart sio kulea lea UOZOOO


Nawasilisha kwenu wadau kama na ww ulikutana na kisa cha namna iyo share ili wadau wa Udart wajue
 
Ni wapuuzi sana mimi nimeona zaidi ya mara mbili pia,
 
Wanaringia ajira walizonazo wakisahau abiria ndio waliowapa ulaji huo
 
Africa customer care ni 0,si udart sehemu nyingi tu za kazi kuna mafala wanafokeana na wateja pasipo kujua hao wanaowafokea ndio wanaweka mjini
 
Africa customer care ni 0,si udart sehemu nyingi tu za kazi kuna mafala wanafokeana na wateja pasipo kujua hao wanaowafokea ndio wanaweka mjini
Na kibaya zaid wanacho ringia si kuna ile by law inayokataza mtu kupiga picha ktk kituo cha mwendokasi so wanajua watamjibu mteja watakavyo jisikia then hakuna kitakacho onekana nje
 
Kuna jamaa cjui tiket alijisahau akaichana ilihali haijakaguliwa na mkagua teketi basi ikawa ni ubishi mwanzo mwisho

Kiukweli hivi vitu Tanzania ilikuwa bado Sana sema tunaiga Sana
Wangetuacha tuendelee kupambana na matatu yetu.
 
Back
Top Bottom