meemi
Member
- Mar 19, 2021
- 6
- 1
Takribani mwezi mmoja wakazi wa kata ya Kawe tunataabika na kero ya kukatika maji kiasi bila sababu yoyote ya msingi jambo linalotishia mlipuko wa magonjwa kama kuhara na kipindupindu kutokana na uchafu huku wahusika wakikaa kimya na viongozi wa serikali ya mtaa kutoshughulika na kero hii.
Mbaya zaidi ni pale tunapoona maeneo ya jirani kama Mbezi Beach na Kambi ya jeshi ya lugalo maji yakitoka kama kawaida ila wakazi wa Ukwamani wakihangaika na madumu machafu na mikokoteni ya maji inayobeba maji kwa gharama kubwa ambazo wananchi hatuwezi kumudu, takribani mwezi mzima sasa.
Ni jambo la kushangaza sana kwa karne hii jiji kubwa kama la Dar es salaam kukosa huduma muhimu ya kijamii kama maji.
Tunaomba wahusika washughulikie jambo hili limekuwa kero kubwa
MREJESHO:DAWASA: Kuendelea kwa matengenezo ya umeme katika mitambo ya maji ya Ruvu juu na Ruvu chini