KERO Kero ya Maji Lukobe - Morogoro

KERO Kero ya Maji Lukobe - Morogoro

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Salaam, kwa namna ya pekee naomba kuwasilisha kero yangu kuhusu upatikanaji wa maji manispaa ya Morogoro.

Kumekuwa na utaratibu wa maji kutoka kwa siku, napo kwa masaa machache. Ni ajabu kwasababu Morogoro ni mkoa ambao una vyanzo vingi sana vya maji, lakini wananchi wa manispaa ya Morogoro wanatumia maji ya bwawa la mindu licha ya idadi ya wananchi kuongezeka maradufu kadri siku zinavyozidi kuongezeka.

Kata ya lukobe walikuja kusambaza mabomba, lakini mwaka umepita bila maji, tukiuliza wanasema maji hayawezi kufika Lukobe kwasababu MORUWASA mitambo yake haina nguvu kufikisha maji mpaka lukobe, ni huzuni.

Baadhi ya wanachi wanashangaa kuwa kuna maeneo nchini watu wanapata maji kila siku masaa yote. Wito wangu, serikali itusaidie kuanzisha miradi mikubwa ya maji majispaa ya Morogoro kwani no aibu makao makuu ya mkoa kuwa na shida ya maji.

Pia gharama za kununua maji kila siku tuzitumie kufanya maisha mengine
 
Back
Top Bottom