KERO Kero ya Maji na Umeme Kahama

KERO Kero ya Maji na Umeme Kahama

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Jamaludin

Member
Joined
Apr 26, 2024
Posts
48
Reaction score
40
Mimi ni mkazi wa Kahama Mjini, na ningependa kuwasilisha malalamiko kuhusu sekta mbili: Kahama Urban Water Supply (KUWASA) na Tanesco Kahama.

Huduma ya umeme imekuwa kero, kwani umekuwa ukikatika mara kwa mara bila taarifa maalum, hadi mara 5-9 kwa siku. Hali kadhalika, huduma ya maji pia imekuwa na changamoto; maji yanakatika na kurudi mara 5-8 kwa mwezi, na wakati mwingine hadi mara 4 kwa mwezi. Changamoto hii ni kubwa sana, hasa ikizingatiwa kuwa Watanzania wengi tunategemea huduma hizi kwa mahitaji ya kila siku. Ingekuwa vyema kuwepo na taarifa maalum kwa wananchi ikieleza siku ambayo kutakuwa na ukosefu wa maji au umeme.

Naziomba wizara husika kuingilia kati na kutatua changamoto hizi kwa haraka. Maeneo yanayoathirika zaidi ni Malunga, Lugela, Nyashimbi, Shunu, Nyahanga, Manzese, Igomelo, Majengo, Mhongolo, Mbulu, Nyakato na kwingineko.

Ahsante.
 
Back
Top Bottom