KERO Kero ya Samaki kufungashiwa ndani ya mabasi ya abiria safari za usiku kutoka Mwanza kwenda mikoa mingine

KERO Kero ya Samaki kufungashiwa ndani ya mabasi ya abiria safari za usiku kutoka Mwanza kwenda mikoa mingine

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Very poor

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2020
Posts
405
Reaction score
599
Habari Wanajukwaa,
Naleta hili kama mdau na msafiri wa mara kwa mara. Tumekuwa tukishuhudia tabia isiyofaa kutoka kwa baadhi ya mabasi ya abiria yanayofanya safari za usiku kutoka Mkoani Mwanza kuelekea mikoa mingine.

Baadhi ya haya mabasi yamegeuka kuwa “madaladala ya samaki” usiku. Unakuta junia/gunia za samaki wabichi zimepakiwa chini ya viti, kwenye njia za kupitia, au hata juu ya mizigo ya abiria.

Hali hiyo hupelekea, Harufu mbaya hadi unapata kichefuchefu, Fikiria kusafiri saa 10+ kutoka Mwanza kwenda Dar/Moshi huku basi linanuka samaki. Watu wanatapika, wengine wanashindwa kulala.Uchafu na kuharibu mizigo, Maji ya samaki yanatiririka kwenye sakafu, begi lako linalowa na kutobolewa na harufu hata baada ya siku 3.Hatari ya kiafya, Hii ni hatari kwa watoto, wazee na wenye matatizo ya pumu.

Swali la kujiuliza: LATRA wako wapi? Idara ya Uvuvi wako wapi? Afya wako wapi? Kwa nini basi la abiria liruhusiwe kubeba samaki kama gari la jokofu?

Tumelipia nauli ya V.I.P si ya kubeba samaki. Mamlaka husika tafadhali muokoe hadhi ya usafiri wa mabasi Hasa ya safari za usiku.

Nawasilisha.
 
Acha fix na wewe,samaki wabichi wawekwe kwenye gunia?halafu bus gani hilo linabeba samaki wabichi kwenye gunia?na nyie JF sio kila kero mnaleta huku,nyingine tupieni kwenye dustbin.
 
Back
Top Bottom